SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

MKUMBUKE MBUNIFU WA KWANZA
ThrowBack

MKUMBUKE MBUNIFU WA KWANZA 

 

Zelda Wynn Valde Ni mbunifu wa kwanza mwenye asili ya Kiafrica (African-American), Mwanamama huyu alizaliwa 28/6/1905 lakini kwa bahati mbaya alifariki 26/9/2001. Zelda alifungua duka lake mwenyewe broadway katika mji wa New York ambalo lilikua ni duka la kwanza katika eneo hilo kumilikiwa na mtu mwenye asili ya Africa.

o-ZELDA-WYNN-VALDES-facebook

Zelda alikua ni mbunifu mkongwe mwenye asili ya Africa ambae ana duka lake broadway katika mji wa new mwaka 1948, alikua akikuza ujuzi wake kwa kufundishwa na bibi yake pia kufanya kazi na mjomba wake ambae alikua ni mshonaji. Alianza kushona nguo za masanamu (dolls) na baadae kumshonea gauni bibi yake japo bibi yake hakuuamini sana uwezo wa Zelda lakini baada ya kuona gauni alilo mtengenezea alivutiwa nalo.

Zelda kazi yake ya kwanza ilikua katika duka kubwa la nguo ambapo haikua rahisi yeye kuipata lakini alifanya kila jitihada kuthibitisha kuwa anaweza, kwa sababu ya kazi yake nzuri watu wakaanza kumtambua na kuanza kumtaka hata wale ambao hawakua na uhakika nae mwanzoni. Zelda aliweza kufungua maduka yake ya nguo mjini New York na pia midtown manhattan baada ya kuamia huko.

d18763e88b5a4333cf99b27e0aee14c8

Zelda aliwavutia watu maarufu wengi kama Dorothy Dandridge, Joyce Bryant, Ella Fitzgerald na Mae West. Mwaka 1949 Velda alichaguliwa kuwa Rais wa New York Chapter of NAFAD, the National Association of Fashion and Accessory Designers.

Zelda aliajiliwa na hugh Hefner kubuni vazi la kwanza la Playboy Bunny,Akiwa na miaka 65 Zelda alijaliwa na Arthur Mitchell kubuni mavazi kwa ajili ya Dance Theatre of Harlem.

08fcc175582aaac10b0df53701dc8724 slide_279312_2073556_free IMG_5997

 

Amefanya kazi nyingi lakini katika umri wa miaka 83 Zelda ali staafu kufanya ubunifu na alifariki 2001 katika umri wa miaka 96.

Related posts

2 Comments

  1. site

    … [Trackback]

    […] Info on that Topic: afroswagga.com/throwback/mkumbuke-mbunifu-wa-kwanza/ […]

  2. window repair

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/throwback/mkumbuke-mbunifu-wa-kwanza/ […]

Leave a Reply