Buns Za Ufuta
Vipimo
Unga 4 Vikombe vya chai
Sukari 1 Kijiko cha supu
Chumvi 1 Kijiko cha chai
Hamira 1 Kijiko cha supu
Baking powder 1 Kijiko cha chai
Siagi ¼ Kikombe cha chai
Maziwa 1 ½ Vikombe vha chai
Yai 1 Moja
Ufuta Kiasi ya kunyunyizia juu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katika bakuli changanya vipimo vyote isipikuwa ufuta.
- Kisha ukande unga huku unanyunyizia unga ukiwa unashika.
- Funika mchanganyiko na weka pahali penye joto hadi iimuke.
- Halafu fanya viduara na viweke kwenye treya ya kuchomea iliyopakwa siagi.
- Ziache pahali penye joto hadi zimuuke kwa mara ya pili.
- Washa oveni moto wa 350°.
- Pakiza (brush) Yai uliopiga au maziwa juu ya vile vidonge kisha nyunyizia ufuta juu
- Kisha vumbika kwenye oveni kwa muda wa dakika 15 hivi nakuweka moto wa juu hadi ziive na kugeuka rangi na zitakuwa tayari kuliwa
Kuku Wa Karai (Pakistani)
Vipimo
Kuku aliyekatwa vipande vipande – 5 LB
Mafuta – 1 Kikombe cha chai
Nyanya zilizokatwa ndogo ndogo – 5 kubwa
Nyanya ya kopo – 2 kiijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi – 2 vijiko vya supu
Pilipili mbichi (zipasue katikati) – 3 au 5
Bizari ya pilau ya unga (Jeera) – 2 vijiko vya chai
Gilgilani ya unga (Dania) – 1 kijiko cha chai
Paprika – 1 Kijiko cha supu
Bizari ya manjano ya unga – 2 vijiko vya chai
Chumvi – kiasi
Kotmiri iliyokatwa ndogondogo – 1 kikombe kimoja
Pilipili mboga (kijani) – 1
Ndimu – 2 vijiko vya supu.
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Tia mafuta katika karai yashike moto vizuri.
- Tia Thomu na tangawizi kaanga kidogo tu.
- Tia nyanya, pilipili mbichi, nyanya ya kopo na bizari zote.
- Mtie kuku na mkaange katika masala hayo.
- Funika karai na wacha moto wa kiasi, kuku atoe maji yake na apikike.
- Karibu na kuwiva kuku tia pilipili mboga iliyokatwa vipande vipande, kotmiri na ndimu.
- Funua karai na endelea kukaanga mpaka awe anakaribia kukauka, muepue na tayari kuliwa.
Related posts
5 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More on to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/buns-za-ufutakuku-wa-karai-pakistan/ […]
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/buns-za-ufutakuku-wa-karai-pakistan/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/buns-za-ufutakuku-wa-karai-pakistan/ […]
… [Trackback]
[…] Info on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/buns-za-ufutakuku-wa-karai-pakistan/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/buns-za-ufutakuku-wa-karai-pakistan/ […]