Mahitaji
- Unga wa ngano kilo 1
- Mayai 2
- Chumvi kijiko 1 cha chai
- Maji
- Siagi (butter) vijiko 3 vikubwa
- Mafuta ya kula kwa ajili ya kuchomea
- Iliki ya unga kijiko 1 kikubwa
- Maziwa ya unga vijiko 3 vikubwa
Maelekezo
Unaweza kuandaa chapati hizi kisha ukahifadhi na kula wakati unaopenda. Hakikisha umehifadhi vizuri kwenye mifuko laini ya plastic ili iwe na unyevunyevu unaotakiwa.
- Kwenye beseni au sufuria kavu weka unga, chumvi, maziwa vijiko 3 vya chakula na iliki. Changanya pamoja hadi kila kitu kiwe kimechanganyika vizuri.
- Weka siagi vijiko vitatu kwenye mchanganyiko wenye unga kisha changanya zaidi hadi siagi ishikane vizuri na unga.
- Pasua mayai pembeni, yakoroge vizuri na kisha weka kwenye unga. Changanya zaidi hadi upate uwiano unaofaa.
- Ukiona uwiano mzuri wa unga wako, weka maji ya uvuguvugu kwenye unga na anza kukanda. Kanda dida la chapati (mchanganyiko wa unga na maji) hadi uwe laini kabisa na haushikani na chombo unachokandia wala haunati kwenye mikono. Hapo unga utakua tayari kukupa chapati laini na tamu. Hii inachukua takribani dakika 20.
MUHIMU: Hakikisha unga umekandwa vizuri na umekuwa laini kabla ya kuuacha. Hii ndio hatua muhimu zaidi kuliko zote. Unaweza kuchukua takribani dakika 20 ili kumaliza hatua ya ukandaji, hivyo kuwa na subira ili kupata matokeo mazuri.
- Kata mabonge ya unga kwa umbo la mviringo kisha weka kwenye chombo pembeni. Rudia hili zoezi hadi unga uishe.
- Chukua donge mojamoja, paka unga weka kwenye kibao cha kusukumia chapati, sukuma chapati vizuri hadi iwe na umbo zuri duara bapa. Paka mafuta kwenye chapati na anza kukunja.
- Rudia hilo zoezi kwa madonge yote yaliyobaki. Ukimaliza, anza kusukuma chapati zako kwa ajili ya kupika.
- Bandika kikaango jikoni. Acha kipate moto vizuri.
- Weka chapati, acha iive hadi iwe rangi ya kahawia. Geuza upande wa pili, paka mafuta kidogo sana upande uliokua wa kahawia kwa kutumia kijiko huku ukisambaza vizuri yaenee chapati nzima. Geuza, paka mafuta tena upande mwingine. Mafuta husaidia kuifanya chapati iwe laini na isipasuke kirahisi. Hii itasaidia kupata chapati tamu na laini, hasa wakati wa kula.
- Hakikisha chapati inaiva vizuri na inachambuka.
- Rudia zoezi hili hadi dida lako liishe. Hapo utakuwa umemaliza kazi na tayari kula chapati zako.
- Unaweza kula chapati hizi na vyakula aina tofauti, mfano unaweza kula na mchuzi mtamu, chai, vinywaji baridi na vingine. Jirambe na chapati tamu.
Samaki Wa Kupaka
Vipimo
Vitu Vya Samaki
Samaki mkubwa wa chango – 1
Thomu na Tangawizi iliyosagwa -1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagawa -1 kijiko cha supu
Bizari ya pilau ya unga – ½ kijiko
Ndimu – 1 kamua maji
Chumvi-kiasi
Vitu Vya Rojo
Vitunguu maji – 2
Nyanya – 2
Tuwi la nazi zito – 1 ½ kikombe
Nyanya ya kopo – 1 kijiko cha chai
Bizari ya manjano – ½ kijiko cha chai
Pilipili mbuzi – 1 au mbili
Ndimu – 1 kamu maji
Chumvi – kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na KupikA
- Mroweke samaki kwa viungo hivyo kisha muweke katika tray na mchome (grill) katika jiko (oven), akiwiva upande mmoja mgeuze upande wa pili.
- Saga vitunguu na nyanya kidogo tu kwa kutumia tui kidogo katika mashine (blender). Na ukipenda iwe kali zaidi tia pia pilipili mbuzi moja, kisha mimina katika sufuria utakayopikia.
- Tia tui na bizari zote pamoja na nyanya ya kopo, chumvi, pilipili mbuzi nzima na pika moto mdogo mdogo.
- Rojo likianza kuwa zito tia ndimu.
- Epua na mwagia juu ya samaki. Tayari kuliwa.
Related posts
3 Comments
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/chapati-za-maziwa-na-samaki-wa-kupaka/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/chapati-za-maziwa-na-samaki-wa-kupaka/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/chapati-za-maziwa-na-samaki-wa-kupaka/ […]