SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Ndizi Mzuzu
Uncategorized

Ndizi Mzuzu 

Ndizi ni moja kati ya chakula kinacholiwa sana katika futari, walaji huwa wanachanganya na mihogo na magimbi kutoa mchanganyiko wa Futari, Leo katika Futuru yako tutakueleza namna ya kuandaa Ndizi Mzuzu ambazo zinaungwa kwa tui la nazi. Zifuatazo ni mahitaji na hatua zitakazokuwezesha wewe kujipikia futari hii ya Ndizi Mzuzu.

Ndizi mzuzu


MAHITAJI

 • Ndizi tamu (plantain) 3-4 inategemea na idadi ya watu
 • Tui la nazi (coconut milk) kikombe 1 cha chai
 • Sukari (sugar) 1/4 ya kikombe cha chai
 • Hiliki (Ground cardamon) 1/4 ya kijiko cha chai
 • Chumvi (salt) 1/4 ya kijiko cha chai

MATAYARISHO

Menya ndizi kisha zikwangue utomvu wote. Baada ya hapo zikate kati (kiurefu) na kisha kata tena kati katika kila ndizi vitoke vipande 4. baada ya hapo toa moyo wa katikati wa ndizi. Zioshe na kisha zikaushe maji na uziweke kwenye sufuria ya kupikia. Baada ya hapo tia tui la nazi, sukari, chumvi na hiliki. Ziinjike jikono na uziache zichemke uku ukiwa unalikoroga tui ili lisikatike. Baada ya dakika 10 tui la nazi litakuwa limepungua na kubaki kidogo na hapo ndizi zitakuwa zimeshaiva. Ziache zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa. Zinaweza kuliwa kama mlo (main meal) au kitinda mlo (dissert) au mlo wa pembeni (side dish) haswa kwa futari,pia unaweza kuliwa na tambi,losti maini au mboga yoyte ya mchuzi.
Imetayarishwa na Afro Swagga Magazine|Picha: Fauzia M. Afif

Related posts

3 Comments

 1. Bubble Tea

  … [Trackback]

  […] There you can find 51667 more Information to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/futari-ya-ndizi-mzuzu/ […]

 2. click through the following web page

  … [Trackback]

  […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/futari-ya-ndizi-mzuzu/ […]

 3. 티비위키

  … [Trackback]

  […] Information on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/futari-ya-ndizi-mzuzu/ […]

Leave a Reply