Urojo-Zanzibar_jpg-3

Mahitaji:

viazi mviringo/mbatata – kg1

unga wa ngano – 1/2kg (nusu kilo)

binzar (rangi ya mchuzi) – kijiko kimoja

malimao au ndimu – 4

chumvi kiasi

maji ya kutosha kulingana na mahitaji

kidokezo:Unaweza kuongeza vitu vya ziada kama nyama au mboga mboga kulingana na mahitaji yako

Mandaalizi:

  1. Safisha viazi mbatata/ mviringo bila kumenya kisha vichemshe, chemsha hivyohivyo    bila kumenya hakikisha havivurugiki vikiiva ipua na uviweke pembeni,
  2. Bandika sufuria lingine la maji huku pembeni ukikoroga unga wa ngano uliochanganywa na maji (uji wa ngano) kwenye bakuli, endelea kukoroga unga wa    ngano mpaka uwe mwepesi na usiwe na madonge, kisha weka binzari.
  3. Maji ya jikoni yakishachemka, mimina mchanganyiko wako wa ngano na binzari kwenye maji ya moto             koroga uji wako hadi ushike vizuri uji ukisha shika vizuri kamulia malimao na punguza moto na uuache uji uendelee kuchemka, wakati uji  ukiendelea kuchemka menya vile viazi vyako ulivyo vichemsha mwanzo na uvikate  vipande saizi ya kati kisha vimimine (tumbukiza) katika uji uliopo jikoni. acha mchanganyiko wako uchemke kwa dakika tano kisha ipua urojo wako utakuwa tayari kuliwa.

KIDOKEZO: Unaweza kuchanganya urojo wako na kachori, bagia, mishikaki, crips za viazi  au mihogo iliyo katwa katwa vipande vidogo vidogo PIA unaweza weka mboga mboga (figiri, majani ya kitunguu maji,kabichi) tayari kwa kuliwa.

 

Comments

comments