SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Mbaazi Kwa Maandazi
Uncategorized

Mbaazi Kwa Maandazi 

MAANDAZI

MAANDAZI

Vipimo

Unga  –  5 Vikombe

Tui la Nazi zito vugu vugu – 1 ¼ kikombe

Sukari –  3/4 kikombe cha chai

Samli iliyoyayushwa au mafuta    – 3 vijiko vya Supu

Hamirah – 2 Vijiko vya Supu

Hiliki  –  1/2 Kijiko cha chai

Mafuta ya kukaangia

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1.  Ndani ya kibakuli kidogo, mimina hamira na na vijiko viwili vya   kulia vya tui. Weka kando  mpaka hamira ianze kufura, kama dakika 5-10.
  2. Pasha samli moto
  3.  Ndani ya bakuli kubwa au sinia, changanya unga, sukari, iliki  na   samli ikiwa bado moto moto.
  4. Mimina hamira  ndani ya mchanganyiko wa unga. Changanya na ukande huku ukitumia lile tui la nazi. Tui likipungua unaweza ukaongeza maziwa. Kanda unga mpaka uwe laini.
  5. Kata madonge *12 au 15  uyaweke kwenye baraza iliyonyunyiziwa unga na uyafunike ili yapate kufura na yasikauke.
  6. Madonge yakifura, sukuma kama chapati kisha ukate mara nne kama kwenye picha. Endelea kufanya hivyo na madonge yote. Yawache maandazi yafure tena baada ya kukata kama dakika 15 hivi.

*Ukipenda  maandazi  manene fanya madonge 12.  Ukipenda mepesi fanya madonge 15

  1. Pasha mafuta moto kwenye karai. Maandazi yako tayari kukaangwa sasa.
  2.   Kaanga maandazi kwenye mafuta ya moto. Upande mmoja ukifura na kuwa rangi nzuri geuza upande wa pili. Endelea nama hii mpaka maandazi yote yawe tayari.

Vidokezo: Kuhifadhi Maandazi

  1. Unaweza kuweka unga wa maandazi uliyokwisha kuyakata ndani ya freezer

yakisha umukua  ikiwa unataka kutumia siku nyengine. Tumia waxed paper na unga wa kutosha kuweka katikati ya maandazi ili yasishikane unapoya freeze kwanza katika freezer.  Yakishika barafu, toa na yafunike kwa wax paper kiasi kama matano pamoja na uyatie katika freezer bags.    Ukitaka kukaanga maandazi siku nyengine, toa maandazi mapema kidogo  yatoke barafu kidogo tu.  Pasha mafuta moto kwenye karai na kanga maandazi.

  1. Vile vile unaweza kuyapika kabisa na kuweka katika freezer bags, ukitaka kutumia ni kuyatoa tu na kupasha moto katika Microwave.

 

MBAAZI ZA NAZI

curry-pigeon-peas-recipe-5-300x225

Vipimo

Mbaazi za kopo (pigeon peas) -40 fl oz (vikopo viwili) (Vikombe vitatu)

Ikiwa mbaazi kavu  – 3 Vikombe

Tui la nazi zito  –  1 Kikombe

Kitunguu   –   1

Chumvi kiasi

Pilipili mbichi- 2

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Ikiwa ni mbaazi kavu, roweka katika maji kwa muda wa masaa kisha chemsha hadi ziwive.
  2. Ikiwa ni mbaazi za kopo, mwaga maji yake ya kopo umimine katika sufuria.
  3. Kata vitunguu na utie katika mbaazi.
  4. Tia tui, chumvi, pililipili mbichi upike hadi kwa muda mdogo tu hadi tui lipunguke kidogo, zitakuwa tayari kuliwa.

Related posts

4 Comments

  1. รักษาหนองใน

    … [Trackback]

    […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/mbaazi-kwa-maandazi/ […]

  2. golden teacher mushroom strain effects,

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/mbaazi-kwa-maandazi/ […]

  3. Cheap DMT for sale Victoria

    … [Trackback]

    […] Read More here on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/mbaazi-kwa-maandazi/ […]

  4. 666클래스

    … [Trackback]

    […] Info to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/mbaazi-kwa-maandazi/ […]

Leave a Reply