SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

MEATPIES ZA KIASILI
Uncategorized

MEATPIES ZA KIASILI 

11667390_694077657365051_408641717218335509_n

MEATPIES ZA KIASILI
Mahitaji:-

Nusu kilo nyama ya kusaga/kima
Vitunguumaji 3 vikubwa vikate vipande 4-4
Pilipilimbichi 2 zikate mara nne
Vijiko 3 vikubwa tomato ya mkebe
Konde 2 za thomo
Chumvi vijiko 2 vidogo
Nusu kijiko kidogo pilipilimanga
Nusu kijiko kidogo mdalasini
Na dania nusu kikombe

Kwa Unga wako utahitaji:-
-Kiazi kibichi kimoja
-Kijiko 1 kikubwa Hamira
-Kijiko kimoja kidogo sukari
-Nusu kikombe maji ya vuguvugu
-Vikombe 2 na robo unga wa ngano
-Kijiko 1 na nusu kidogo chumvi
-Na vijiko 2 vikubwa mafuta ya Zeitun.

NAMNA YA KUTAYARISHA NYAMA:-

Kuunda nyama, mimina kila kitu kwenye blender au mashini ya kusaga nyama isipokuwa dania…

Saga vyote hivyo hadi iwe uji uji…

Baadae mimina dania utakayokuwa umeikatakata udogo kwenye huo mchanganyiko na koroga kutumia mwiko…

Baada ya hapo finika mchanganyiko huo kwenye bakuli na hifadhi kwa fridge kiasi ya kuunda unga wa meat pie hizi…

KATIKA KUUNDA DONGE LA UNGA:
Kishambue kiazi na kikate vipande vinne, kisha kichemshe hadi kiive…

Hifadhi nusu ya maji ulIochemshia kiazi, weka kando…

Kwenye kibakuli, kivuruge kiazi hicho kwa kutumia uma hadi kilainike na weka kando…

Kwenye glass moja, changanya hamira, sukari na nusu ya maji vuguvugu, wacha ikae pamoja kwa dakika 5 hadi ifanye povu…

Sasa kwenye bakuli safi, kavu, mimina unga, chumvi, mafuta ya zeitun na kiazi…

Kisha mimina mchanganyiko wa hamira pamoja na maji ya kiazi ulobakisha…

Kanda mchanganyiko huo wa unga kwa dakika 10, unda boli, lipake mafuta juu na chini, kisha lifinike kwa kitambaa , wacha liumuke…

Baada ya lisaa moja, katakata vidonge sawia..na kwa kila kidonge sukuma mfano wa chapatti lakini umbo dogo kiasi, kisha teka kijiko 1 kikubwa cha mchanganyiko wa nyama na pakiza kwa kusambaza juu ya mduara huo…

Utarudia hali hii kwa vidonge na nyama iliyosalia…

Oka mikate hii au meatpie hizi asilia kwa dakiak 10 kwenye umoto wa 225, ukigeuza geuza tray yako baada ya dakiak 5 kuhakikisha mviringo wote unaivia sawia…

Andaa baadae zikishapoa kiasi kwa kinywaji upendacho.

Related posts

5 Comments

 1. check out the post right here

  … [Trackback]

  […] Info on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/meatpies-za-kiasili/ […]

 2. สร้างไลน์ official

  … [Trackback]

  […] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/meatpies-za-kiasili/ […]

 3. BiNANCE £

  … [Trackback]

  […] There you can find 47999 more Information to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/meatpies-za-kiasili/ […]

 4. Pink Zkittlez 3.5g Flower

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/meatpies-za-kiasili/ […]

 5. check

  … [Trackback]

  […] Here you can find 23291 more Info on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/meatpies-za-kiasili/ […]

Leave a Reply