SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

MIKATE YA SINIA/ MIKATE YA KUMIMINA KWA KUKU WA SOSI
Uncategorized

MIKATE YA SINIA/ MIKATE YA KUMIMINA KWA KUKU WA SOSI 

images

Mkate Wa Sinia – Mkate Wa Kumimina

 • 1 KIKOMBE CHA MCHELE
 • 1 KIKOMBE CHA NAZI YA UNGA
 • 1 KIKOMBE CHA SUKARI KUPUNGUA KIDOGO
 • 1 KIKOMBE CHA MAJI AU MAZIWA VUGUVUGU
 • 1 KIJIKO CHA CHAI CHA HAMIRA
 • ILIKI KIASI UPENDAVYO
 • UTE WA YAI MOJA

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Osha na kuroweka mchele siku moja ndani ya maji ya baridi.
 2. Saga ndani ya blender, mchele, tui, maji au maziwa, iliki, na hamira mpaka  mchanganyiko uwe lani kabisa.
 3. Mimina ndani ya bakuli na ufinike. Weka mahali penye joto ili mchanganyiko uumuke(ufure).
 4. Mchanganyiko ukifura, washa oven moto wa 350°. Mimina sukari pamoja na ule ute wa yai ndani ya mchanganyiko na uchanganye vizuri. Ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
 5. Chukua sufuria umimine mafuta kidogo. Washa jiko na uweke sufuria ipate moto kiasi. Mimina ule mchanganyiko ndani ya sufuria uuwache kama dakika 5 hivi kiasi mkate uanze kushikana.
 6. Funika sufuria na uvumbike(bake) ndani ya oven kama dakika 35-40 hivi, au mpaka mkate uive na uwe rangi ya hudhurungi juu yake.
 7. Epua na uwache upoe kabisa kabla ya kukata.

Kuku Wa Sosi Tamu (Trinidad)

8407155311_33ea8edc2a_o

Vipimo  

Kuku – 6 LB

Kitunguu saumu/thomu na tangawizi iliyosagwa   –  2 vijiko vya supu

Mtindi  –    2 vijiko vya supu

Chumvi  –   kiasi

Pilipili nyekundu ya unga   – 1 kijiko cha chai

 

Sosi

Mafuta   – 2 vijiko vya supu

Thomu iliyosagwa  –  1 kijiko cha chai

Sosi ya tomato (tomato sauce)  –   ¼ kikombe

Sosi ya HP   –  2 Vijiko vya supu

Cellery  –  1 mche

Parsley na kotmiri    –  ¼ kikombe

Nyanya –   3

Chumvi  –     kiasi

Pilipili manga  –   1 Kijiko cha supu

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 1. Mkate kuku vipande vikubwa vikubwa, msafishe kwa siki atoke harufu
 2. Mrowanishe na thomu, tangawizi , chumvi, mtindi na pilipili kwa muda wa  saa au zaidi.
 3. Mtie katika tryea ya kupikia katika oveni.
 4. Mchome kwa moto juu (grill) au ukipenda moto wa chini (bake) , akishawiva pakua katika bakuli la kupakulia.
 5. Tengeneza sosi kwa kufanya ifuatavyo:
 6. Saga kwanza Nyanya, cellery, parsely na kotmiri.
 7. Kaaanga thomu katika mafuta kisha tia sosi zote pamoja na mchanganyiko uliosaga wa cellery.
 8. Mwagia sosi katika kuku akiwa tayari kuliwa.

 

Related posts

4 Comments

 1. how long does marijuana stay in your system

  … [Trackback]

  […] Find More on on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/mikate-ya-sinia-mikate-ya-kumimina-kwa-kuku-wa-sosi/ […]

 2. buy golden teacher mushroom online on facebook,

  … [Trackback]

  […] Find More on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/mikate-ya-sinia-mikate-ya-kumimina-kwa-kuku-wa-sosi/ […]

 3. chocolate mushrooms

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/mikate-ya-sinia-mikate-ya-kumimina-kwa-kuku-wa-sosi/ […]

 4. Aquarius boat rental miami

  … [Trackback]

  […] Find More Information here to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/mikate-ya-sinia-mikate-ya-kumimina-kwa-kuku-wa-sosi/ […]

Leave a Reply