SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

SAMBUSA NA MAZIWA YA TENDE
Uncategorized

SAMBUSA NA MAZIWA YA TENDE 

  • sambusaSAMBUSA ZA KUFUKIZA
    Mahitaji:-

    Manda za sambusa za tayari, 20-30
    Nyama ya kima nusu kilo
    Mchanganyiko wa thomo na tangawizi mbichi vijiko 3 vidogo
    Mchanganyiko wa bizari kijiko 1 kikubwa
    Kitunguumaji kimoja kikate udogo
    Dania moja ikate udogo
    Maji ya limau moja
    Chumvi kiasi
    Na mafuta ya kukaangia baadae lita moja

    NA KATIKA KUUNGANISHA SAMBUSA HIZO UTAHITAJI:-
    -Unga wa ngano kikombe kasorobo
    -na maji kiasi.

    JINSI YA KUANDAA:-

    Ipike nyama yako kwanza ya kima kwa kuichapua kwa michanganyiko ya thomo na bizari, imwagilie maji ya limau, vitunguumaji na dania kiasi…

    Ipike nyama hiyo moto wa chini kwa kuikoroga koroga kwa mwiko ili iachane na kuwa moja moja, kusudio likiwa kuipa sura nzuri na iwe rahisi kwako kufunga kwenye manda…

    Ipike nyama hiyo hadi iashirie kukauka, bila ya kusahau chumvi kiasi…

    Iwache ipoe kiasi ya kuunda gundi ya kufungia manda hizo…

    Changanya huo unga na maji kwenye kibakuli hadi upate mchanganyiko mzito…

    Sasa kufukiza kwenyewe kunakuja hivi..:-

    Katika ganda la kitunguu, teua kile kiganda cha ndani, unda kama shimo kwenye sufuria ya nyama na weka hilo ganda,lipakie mafuta kidogo kisha chukuwa kikaa cha moto, kibwage kwenye hilo ganda na mafuta..huo moshi ndio mpango wote..finika hiyo sufuria kwa muda wa robo saa ili moshi utapakae na kuipa nyama yako harufu kama nyama choma…

    Baada ya hapo funga sambusa zako kwa kutumia manda na tayari kuzikaanga…

    Bandika karai motoni, mimina mafuta na yakianza kushika moto zikaange kwa makini…

    Ukitaka kufaidi rangi nzuri sawia kwa upishi huu, moto uwe wa chini na usichome sambusa yakiwa mafuta moto sana

 

 

MAZIWA YA TENDE10345757_691313434308140_3260706352996860703_n

 

 

 

Mahitaji:-

Maziwa nusu litre
Tende habba 7 hadi 11 zilizotolewa konde
Na vidonge vya barafu iwapo utahitaji.

Jinsi ya kuandaa:-

Kwa tende ulozitoa kokwa, ziweke kwenye bakuli safi kwanza …
Kisha tumia maji moto kiasi na umimine juu ya hizo tende, wacha zikae hivyo kwa nusu saa…

Kisha mwaga maji na bakisha tende pekee…

Baadae Kwenye blender, mimina maziwa yote kisha umimine na tende, saga hadi huo mchanganyiko uwe rojo rojo…

Mimina kwenye jagi na waweza zizimua kwa vidonge vya barafu au ukanywa hivyo ilivyo.


 

Related posts

4 Comments

  1. Buy DMT Powder Online Perth

    … [Trackback]

    […] Read More here on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/sambusa-na-maziwa-ya-tende/ […]

  2. ยารักษาหนองใน

    … [Trackback]

    […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/sambusa-na-maziwa-ya-tende/ […]

  3. review

    … [Trackback]

    […] Information to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/sambusa-na-maziwa-ya-tende/ […]

  4. mushrooms for sale online​

    … [Trackback]

    […] Here you will find 29259 more Information on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/sambusa-na-maziwa-ya-tende/ […]

Leave a Reply