VILEJA VYA NAZI
Mahitaji:
Vikombe – 4 nazi aina ya Dessicated
Kijiko – 1 kidogo Vanilla
Kopo moja la Maziwa matamu ya Condensed
Kijiko – 1 kidogo baking powder
Kijiko – 1 kikubwa siagi iyayushe
Na Icing sugar kikombe 1 kwa kupambia.
NAMNA YA KUTAYARISHA:-
Changanya vyote hivyo isipokuwa Icing sugar kwenye bakuli la mashini na usage mchanganyiko huo hadi upate donge laini
Nyambua donge hilo kiasi ya kuuunda vitonge vidogo kasha weka kwenye kalai la kuoka , finyilia kidonge hicho uunde umbo la biskuti
Endelea kufanya hivyo kwa vitonge vyote na panga biskuti hizo kwa kuzipa nafasi kila baada ya nyengine kwenye ilo kalai
Washa jiko la kuoka (oven) umoto wa degrees 175 C na zioke biskuti hizo kwa dakika 15 au 20 au mpaka zianze kubadilika rangi na kua rangi ya kahawia na harufu ya kuvutia
Ziache zipoe kiasi ndipo sasa uzihifadhi kwenye sahani na kwa kutumia kichujio, nyunyizia icing sugar kwa juu kwa kupambia
Zihifadhi kwenye mkebe kwa kuchelea kulainika kwa upepo na vile vile kudumu kwa wiki…
Nakutakia matayarisho mema ya Eid
Related posts
1 Comment
Leave a Reply Cancel reply
You must be logged in to post a comment.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/vileja-vya-nazi/ […]