SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

VITUMBUA KWA MCHUZI WA KAMBA
Uncategorized

VITUMBUA KWA MCHUZI WA KAMBA 

Amani 2006 027

 

Vitumbua

Mahitaji na vipimo

 • mchele kilo 1
 • nazi kubwa 2
 • hiliki kiasi
 • sukari robo kilo
 • hamira kiasi kijiko kimoja nusu ( itategemea aina ya hamira)
 • mafuta nusu lita
 • mayai 3 (ukipenda)

namna ya kupika

 1. uroweke mchele uliokwisha uchambua vizuri na kuupeta.
 2. utandaze sehemu safi ukauke, kisha usage upate unga mlaini
 3. kuna nazi uchuje tui zito
 4. saga hiliki, changanya na sukari
 5. changanya ule unga wa mchele, sukari, hiliki, tui la nazi na hamira. uvuruge uwe mwepesi kiasi cha kuweza kuchoteka kwa upawa. Acha uumue kwa dakika 25 hadi 30 kutegeme na ubora wa hamira.
 6. weka kikaango cha kukaangia vitumbua jikoni, anza kukaanga vitumbua vyako kwa kueka mafuta kwanza yapate moto, kisha unachota kwa upawa unga na kueka kwenye vijungu vya kikaangio chetu. unaacha vichemke upande mmoja, kisha unageuza upande wa pili, vikishaiva vitoe weka kwenye chujio ili mafuta yajichuje. Endelea kukaanga viliobakia mpaka unga uishe

vitumbua hivi vinaweza kuliwa na chai, maziwa, uji na hata juice ukipenda na mchuzi.

 

MCHUZI WA KAMBA

s-prawn-roast

Vipimo

Viazi (mbatata)  – 2

Kamba  – 1 Lb

Vitunguu – 2

Nyanya  – 2

Pilipili hoho – 1

Kitunguu saumu – 1 kijiko cha chai

Tangawizi – 1 kijiko cha chai

Uzile (bizari ya pilau ya unga-Jiyra)  – ½ kijiko cha chai

Pilipili manga –  ½ kijiko cha chai

Pilipili ya unga – ½ kijiko cha chai

Nyanya ya kopo – ½ kijiko cha chai

Chumvi –  kiasi

Namna Ya Kutayarisha

1)       Changanya kamba na  thomu, tangawizi, pilipili manga, pilipili ya unga, jira na chumvi.

2)      Katakata vitunguu weka pembeni.

3)      Katakata pilipili hoho weka pembeni.

4)      Katakata Nyanya weka pembeni.

5)    Menya viazi na uvikate vidogo vidogo.

Namna Ya Kupika

1)       Kaanga kamba mpaka wabadilike rangi, watie kwenye bakuli.

2)       Kaanga viazi mpaka viwive na vibadilike rangi, vitoe, mimina kwenye bakuli.

3)       Kaanga pilipili hoho viwive na vibadilike rangi, vitoe.

4)       Kaanga vitunguu mpaka vibadilike rangi, mimina nyaya kaanga pamoja, kisha tia nyanya ya kopo na chumvi

5)       Endelea kukoroga.

6)       Mimina maji kama robo kikombe, ukishawiva vizuri, mimina katika bakuli la mchanganyiko na ukoroge kidogo ili vichanganyike tayari kwa kuliwa.

 

Related posts

5 Comments

 1. click for source

  … [Trackback]

  […] Read More on to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/vitumbua-kwa-mchuzi-wa-kamba/ […]

 2. ufabet24h

  … [Trackback]

  […] Read More to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/vitumbua-kwa-mchuzi-wa-kamba/ […]

 3. best microdose mushroom

  … [Trackback]

  […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/uncategorized/vitumbua-kwa-mchuzi-wa-kamba/ […]

 4. mushroom growing kits psilocybin oregon​

  … [Trackback]

  […] Read More here on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/vitumbua-kwa-mchuzi-wa-kamba/ […]

 5. ufabtb

  … [Trackback]

  […] Read More on that Topic: afroswagga.com/uncategorized/vitumbua-kwa-mchuzi-wa-kamba/ […]

Leave a Reply