SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

4 Tips To Level Up Your Hygienne
Urembo

4 Tips To Level Up Your Hygienne 

Hakuna kitu kinaudhi au kukera wengine kama uchafu, iwe kinywa, makwapa au hata mazingira machafu yanakera. Inawezekana pia una jitahidi sana kujisafisha lakini hufikii lengo unalolitaka leo tunakuletea Tips ambazo zinaweza kukusaidia ku-level up hygienne game yako.

Sugua Makwapa Mara Mbili

Kama ambavyo inashauriwa ukiwa unaosha uso u-double cleanse basi kuoga napo ni hivyohivyo, hakikisha unaoga mara ya kwanza na sabuni kisha rudia tena, hakikisha unasugua makwapa mara mbili ili mara ya kwanza ni kuondoa zile layers za perfume na jasho na mara ya pili ni kulisafisha zaidi,

Note: unaweza kutumia sabuni ya kipande mara ya kwanza na mara ya pili ukatumia body wash au ukatumia sabuni inayo nukia hii itakupa harufu nzuri mwilini

Piga Mswaki Mara Mbili Kwa Siku

Kama unaoga asubuhi na jioni basi piga mswaki mara mbili pia asubuhi na jioni, kama unatatizo la kunuka kinywa basi itakusaidia kupunguza tatizo hilo kwa kiasi kikubwa lakini pia hata kama huna tatizo hili ni vyema ukapia mswaki mara mbili ili kuweka hali ya kinywa chako sawa.

Osha Nywele Weekly / Kila Baada Ya Week Mbili

Nywele nazo hunuka unaweza ukaoga vyema, ukapiga mswaki vyema lakini bado ukajishtukia una kiharufu personal kumbe ni nywele, iwe ni nywele asilia, rasta, wig au weaving hakikisha unazisafisha kila week na ikishindikana basi mara mbili kwa week hii itakusaidia kuwa smart.

Badilisha Mavazi ya Ndani Daily

Tunajua boxer na chupi mnajitahidi kubasilisha tatizo ni hizo vest na sidiria, hizo nazo zinashika uchafu perfume juu ya perfume na majasho ya kila siku lazima zitavunda, jaribuni kubadilisha mara kwa mara hata kama sio kila siku basi hata kila baada ya siku mbili.

Tutakuja na mengine lakini tumabie pia ni nini huwa unafanya kuwa fresh siku zote?

Related posts