SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

5 Body Parts Yo Should Clean This Weekend
Urembo

5 Body Parts Yo Should Clean This Weekend 

Weekend ni ule muda wa kujijali (selfcare) na ni kawaida yetu kukumbuka kujifanyia usafi sehemu mbalimbali za miili ikiwa ni kutengeneza nywele, kucha, skin care, kufua mavazi etc. Lakini kuna sehemu kadhaa za mwili huwa tunasahau kusafisha na tupo hapa kukumbusha sehemu hizo na kwanini uzifanyie usafi weekend hii.

  • Kitovu

Wengi huwa tunasahau kusafisha kitovu kwa namna moja au nyingine ni sehemu ambayo haionekani hasa weekdays tunavaa mavazi marefu kinafichika lakini imagine weekend unataka kwenda out uvae crop top halafu kitovu kichafu, girl makeup popi’n, una wig ya maana, dress code on point then mtu anaangalia kitovu kichafu (shame). Lakini ukiachana na hayo hata kama huvai crops unaweza kusababisha bacteria na tunajua kitovu ni sehemu sensitive, kisafishe leo.

Chini Ya Maziwa

Hii ni sehemu nyingine ambayo wengi huwa tunasahau kusafisha, kwakuwa na yenyewe haionekani basi huwa hatuichukulii maanani, lakini ni vyema ukasafisha vizuri chini ya maziwa na kupakausha vizuri pia unaweza kupata fungus kama hupakaushi au kupaacha pachafu.

Masikio

Iwe nyuma ya masikio,ndani ya masikio au kwenye vitundu vya masikio hakikisha una safisha sikio zima, haileti picha nzuri kuwa na sikio chafu na kwenye matundu ya sikio mara nyingi huwa panatoa harufu kama hapasafishwi, unakutana na watu wanakuhug wanaondoka na harufu, please pasafishe this weekend.

Nyuma Ya Shingo / Magoti

Unavaa zako short skirt/pant na off shoulder top lakini huku nyuma magotini na mgongoni kunaonekana kuchafu haileti picha nzuri unaonekana unavaa vyema lakini hujui kujisafisha hakikisha umesugua ondoa uchafu wote na paka mafuta.

Well tuambie hapo chini ni sehemu gani nyingine muhimu kufafisha?

Related posts