SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

ASPIRIN FACE MASK KWA NGOZI AINA MBALI MBALI
Skin Care

ASPIRIN FACE MASK KWA NGOZI AINA MBALI MBALI 

Ukiachana na kuwa dawa nzuri ya kutuliza maumivu, aspirin ina sifika kwa kuwa ni tiba nzuri ya ngozi. Vidonge hivi vinavyo sifika katika kutuliza homa, kichwa au maumivu yoyote pia ina sifika kuwa ni tiba ya ngozi. Kama utakuwa una tumia dawa hizi mara kwa mara katika urembo una weza kupata ngozi yenye afya na nyororo, hii ni kwa sababu aspirin ina acid itwayo acetylsalicylic ambayo husaidia kutibu sehemu iliyoathirika, japo kuwa na sifa hizo lakini pia ina hitajika kuwa muangalifu wakati wa matumizi, kizuri kuhusu aspirin ni kwamba mtu mwenye ngozi ya aina yoyote ana weza kutumia

Aspirin kwa sensitive skin

 • vidonge vinne vya aspirin
 • plain yogurt (mtindi) vijiko viwili

pondaponda aspirin zako mpaka upate ule unga unga kisha changanya na vijiko viwili vya mtindi, paka katika uso wako na uache ikae kwa dakika 15, kisha futa mask hio kwa kutumia kitambaa chenye unyevu, aspirin husaidia kufungua vitundu vilivyo zibwa wakati mtindi una mosturize ngozi yako. mchanganyo wa vitu hivi una weza kusaidia ngozi yako na kuing’aza

Aspirin na limao kwa ajili ya kusafishia ngozi

 • vidonge vinne vya aspirin
 • vijiko viwili vya limao

weka vijiko viwili vya juice ya limao kisha ingiza vidonge vya aspirin vyote, vichanganye mpaka viyeyuke kisha paka usoni kaa nayo kwa muda wa dakika 10 na osha kwa maji masafi. Hii husaidia kusafisha ngozi na huondoa madoa.

Aspirin kwa ajili ya kutibu chunusi

 • vidonge vitatu vya aspirin
 • asali kijiko kimoja
 • maji kijiko kimoja

changanya maji na aspirin mpaka vidonge viyeyuke kisha ongezea kijiko kimoja cha asali, paka usoni kwa dakika 10, kisha ufute baada ya kufanya hivi utaona black heads na wahite heads zilizo kuwepo usoni zimekauka.

aspirin facial mask kwa ajili ya kung’aza ngozi

 • aspirin vidonge vitatu
 • apple cider vinegar kijiko kimoja
 • maji vijiko vinne

dillute vidonge vyako na maji mpaka vitakapo yeyuka, ongezea apple sider vinegar na paka usoni, kaa nayo dakika 10 kisha ondoa utapata ngozi nga’vu

aspirin kwa ajili ya ngozi yenye mafuta

 • aspirin – vidonge vitatu
 • maji – kijiko kimoja
 • tea tree oil -3-4 drops

saga aspirin zako mpaka upate unga unga kisha changanya maji na tea tree oil pamoja na unga wa aspirin, paka na ufute/osha uso baada ya dakika 20

aspirin kwa ajili ya ngozi kavu

 • aspirin – vidonge vitano
 • asali -kijiko kimoja
 • almond oil – 3 mpaka 4 drops
 • maji – kijiko kimoja

saga aspirin zako mapak upate unga unga, weka maji, asali na almond oil, paka mchanganyiko wako usoni kwa dakika 20, kisha nawa uso kwa maji ya vuguvugu

kama utajaribu husisite kutuandikia matokeo kupitia

Instagram – afroswagga

Facebook – afroswaggamag

Twitter – afroswaggatz

 

 

 

 

 

 

 

Related posts

Leave a Reply