SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Athari Za Msongo Wa Mawazo Katika Muonekano Wako
Afya

Athari Za Msongo Wa Mawazo Katika Muonekano Wako 

ee unajua kuwa msongo wa mawazo unachangia mafuta yako kugoma na uso wako kujaa chunusi kwa wingi. Kila mmoja ana mtazamo wake kuhusu msongo wa mawazo ama kama inavyojulikana sana “ stress”. wengine wana stress za maisha, maradhi, ugonjwa, masomo na mambo kadha kadha. kwa kifupi kila mmoja na maana yake. 

Hapa utajifunza ukiwa na stress ni nini kinatokea hadi unahisi kuchoka, huna hamu ya kula ama hamu ya kula inaongezeka zaidi, unahisi hasira wakati wote na mbaya zaidi unapata chunusi na yale mafuta yako mazuri unayopaka usoni siku zote yanagoma.

kwenye mwili kuna vichocheo “homoni” tofauti tofauti ikiwemo homoni ya msongo wa mawazo iitwayo Cortisol humwagwa katika damu pale tu unapoingia kwenye mstuko wa kimawazo.

Athari za homoni hii mwilini Hutegemea sana Muda ambayo homoni hii inadumu kwenye damu na Kiwango cha kuisisimua (Mara kwa mara). Kwa hio kama una ingiza mwili wako kwenye msongo muda mwingi ndivyo unavyopata athari za Homoni hii.

Homoni ya msongo inapomwagwa kwenye damu hukaa kwenye damu kwa dakika hadi 100 karibia masaa mawili ndipo inamaliza nguvu na kuondolewa. Ina maana muda wote huo inaleta madhara mwilini.

Mawazo Yanaweza Kukufanya Muda Wote Homoni hii ikiendelea Kuleta madhara. Na kumbuka Ikisha temwa haiondoki au kushuka hapo hapo. Inadumu muda wote huo ikileta athari mwilini. Kiafya haitakiwi uwe unaisisimua mara kwa mara hadi sababu maalumu mfano Umekutana na nyoka au unataka kumkimbia adui anayetaka kukukata panga nk.

.

Msongo wa Mawazo kwa sababu unasabisha mvurugiko wa homoni ndio unasababisha Chunusi ndogo, na wengine hutoka chunusi kubwa zaidi, na kwa sababu hiyo hiyo ndio hata ukipaka mafuta yanakukataa. yaani hayaendi kufanya kazi yake kama mwanzo maana wewe umeshaharibu mfumo mzima wa upokeaji wa kipodozi husika kwa kuwa mawazo uliyonayo yanapandisha homoni ya mawazo yenye kuleta mvurugiko wa homoni na madhara mengine ni kama ifuatavyo

1. Unaongeza Uzito kwa kasi

2. Msongo wa mawazo unashusha nguvu za kiume

3. Msongo wa mawazo unapandisha sukari na presha

4. Msongo wa mawazo unavuruga homoni za kike

5. Msongo wa mawazo unapanua moyo na kuleta shambulio la moyo

6. Msongo wa mawazo unaweza kukufanya ufikirie kujiua

7. Msongo wa mawazo Unakukosesha marafiki hata wazuri.

8. Msongo wa mawazo unafanya hata nywele zako ziwe zinakatika katika kwa sababu ya mvurugiko wa homoni.

Suluhisho:

Jitahidi kwa namna yoyote unayoweza kujilinda na msongo wa mawazo “ stess” utakuwa salama kwa afya yako na ngozi yako kwa ujumla!

©️binturembo

Related posts

3 Comments

  1. Source

    … [Trackback]

    […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/athari-za-msongo-wa-mawazo-katika-muonekano-wako/ […]

  2. 코인커뮤니티

    … [Trackback]

    […] Find More here on that Topic: afroswagga.com/urembo/athari-za-msongo-wa-mawazo-katika-muonekano-wako/ […]

  3. https://www.advantageja.eu/supplements/phenq-reviews-know-ingredients-pros/

    … [Trackback]

    […] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/athari-za-msongo-wa-mawazo-katika-muonekano-wako/ […]

Comments are closed.