Swahili fashion week imeisha tumepata na nafasi ya kuona vingi ikiwepo wabunifu wameleta collection gani, nini tumependa, waandaaji wametuandalia nini, wanamitindo wana kipya kipi? It was a great experience kwa kweli and very refreshing kwa wapenda fashion. Tumeona vingi vimekuwa improved lakini bado kuna vichache ambavyo tumeona havikukaa sawa well lets start ku-mention vile ambavyo tumeona siku hizi tatu za event hii ikiwa huu ni mwaka wake wa kumi na moja tangu ianzishwe we expected every thing to be proper
- Sehemu Ya Red Carpet Ni Ndogo & Media Awareness
Red carpet ilikuwa ndogo mno hawawezi kusimama watu zaidi ya watatu kupiga picha kwenye red carpet, ilikuwa msongamano watu wanataka wapige picha lakini sehemu ndogo, watu wa media nao wanataka interview hapo hapo basi ni mvurugano. Hawa wanaongea na kuulizana maswali huku wengine wanatak kupiga picha basi alimradi sehemu haitoshi, Kingine ni Media Awareness katika miaka hii 11 ya Swahili Fashion Week na jinsi teknolojia ilivyokuwa tulitegemea tupate picha nzuri kutoka kwa wapiga picha mbalimbali siku hio hio ya tukio, lakini tofauti na matarajio yetu,media zilikuwa chache sana, kwenye red carpet ukipita unakuta mpiga picha mmoja au wawili na kama umechelewa ndio hukuti kitu kabisa, we need to shout media zije, tupate picture za red carpet mapema hii itasaidia kupata awareness kwa watu wengine na hatimae tukafika hadi kwenye magazeti makubwa, ni matumaini yetu mwakani mtajiandaa vyema sio tu kwa kusubiri media za watu mnaweza kuwa na wapiga picha wenu ambao kazi yao ni kupiga picha na kuzisambaza picha kwa wengine.
- Show Kuchelewa Kuanza
Siku ya pili na ya tatu ilikuwa afadhali lakini siku ya kwanza ilikuwa worse tumesubiri kwa lisaa limoja na nusu, wenye makeup zikaanza kuharibika, hii ikapelekea show kuchelewa kuisha, inawezekana bado waandaaji hawakuwa tayari katika kupanga baadhi ya vitu but its better to wake up early na kuanzaa kuandaa jukwaa ili show ianze kuliko kuwawekesha wageni waalikwa, hii tabia inapelekea wageni waalikwa ku-adopt the same behavior na wao kuchelewa, wakichelewa na kupitiliza moja kwa moja ndani inasababisha media watake kupiga picha kipindi wanatoka na hii ndio inaleta mtafaruku kwenye ile point yetu ya kwanza ya red carpet, kama mngekuwa on time na wao wangewahi kuja na sehemu ikawa kubwa ingekuwa rahisi kupata picha na kuzisambaza mapema.
- Mpangilio wa viti
Okay the decor it self was on point, lakini tatizo likaja pale ukitaka kunyanyuka kwenda maliwatoni au kuondoka nafasi ni ndogo sana ya kupishana kupita, inawalazimu wale waliokuwa wamekaa wasimame kumpisha apitae, lakini pia what happened na usher’s kujakuuliza kuhusu vinywaji? inabidi mtu aamke kwenda kufuata au awaite vitu ambavyo vyote havifai katika event kama ile haiitaji kelele wala watu kunyanyuka nyanyuka.
- Mc Hasikiki
Day 1 na 2 ilikuwa hatari ilikuwa shida kumsikia Mc nini kinafuata au nani ameshinda award gani ni kutokana na rafudhi yake lakini pia sauti ilikuwa ndogo, seriously ilikuwa inatupa shida kupost na ku-update watu kuhusu event kwenye page zetu za social media, next time mtuletee mtu ambae anasikika kama Taji ambaye alikuwapo siku ya kilele au muwe mnaonyesha kwenye screen majina ya washindi na mpaka sasa siku ya tatu bado hakuna hayo majina kwenye blog yenu, like seriously?
Kwa wanamitindo
- Catwalk & serving faces
hatujui tuongee mara ngapi kuhusu hili swala, tunahitaji up comings models yes lakini mnapopewa nafasi hamzitumii, tunaweza kusema models mna disappoint wabunifu, yaani majua nyinyi ndio wauzaji wa vazi pale juu mtu anatakiwa kuona linavyo valiwa ndio apende amtafute mbunifu, you don’t carry hizo nguo, mnatembea regular, faces ndo kabisa hamna kitu plain kama uji wa sembe, nothing yaani ni disappointment. Platform kama ile ndio wengine mnapopata kuchaguliwa kupata sponsorship au kazi na makampuni halafu unaenda pale unatembea kama upo kwenye kujifunza do you real want to be international? au mnataka kuishia hapo hapo Swahili Fashion Week? you people need to step up you’re game.
Kwa wabunifu – tunapenda kusema you people have done a marvelous work kwenye mavazi mwaka huu, finishing zilikuwa on point, designs chache sana ambazo tumeona zimejirudia, uniqueness ya fabrics, ilikuwa raha kuangalia collection after collection lakini bado kuna mapungufu
- Matumizi ya stylist
Bado tunapigia kelele hili swala please jamani tumieni stylist, show us pieces zenu in a different way. A stylist can take that collection from 90% to 150% jaribuni kufanya collaboration nao tuone tutapata nini, a collection nzuri yes lakini haina chachu, hamna namna tofauti ya kuvaa, accessories ndio hata tatujui tusemeje collection inaletwa plain hai-standout, viatu ndo kabisaaa hatuji lini mtakuja kutusikiliza mnaweza kusema mnaomba duka livalishe viatu models kwenye collection yetu kwa return ya ku-credit, viatu na accessories vinaweza kubeba na kuharibu muonekano as you present your collection to the people you don’t want to take a risk ya kumwambia model avae viatu vyovyote.
- Makeup & hair stylist
Kama mbunifu you have to have a makeup & hair stylist atakae wa makeup model’s kwenye collection yako, tujaribu ku-spend pesa jamani ili tupate kuitwa huko nje ku-show case hizi collection sio wote kusubiri hii platform hatupigi hatua, models wanakuja na nywele mbaya, make up haieleweki, viatu ndo kabisa, zero styling do we ever learn kutoka kwa wenzetu? darling wapo, prima wote wanatafuta kupata watu wa kutangaza bidhaa zao tunashindwa kugonga hodi huko jamani for the sake of presenting a better collection? Mnadhani Chanel au Gucci wamefika walipo kwa kuwa regular? we hope next year tutaona mabadiliko.
well hio ndio barua yetu na hayo ndiyo tuliyoyaona otherwise kwa mengine yalikuwa vizuri tu tuseme it was 75% nice of a show.
Related posts
2 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/barua-ya-wazi-kwa-waandaji-wanamitindo-na-wabunifu-wa-swahili-fashion-week-2018/ […]
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/barua-ya-wazi-kwa-waandaji-wanamitindo-na-wabunifu-wa-swahili-fashion-week-2018/ […]