SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Beauty Looks Spotted Last Week
Urembo

Beauty Looks Spotted Last Week 

Kuna ule msemo unasema face card never decline, week hii tumeona watu maarufu wengi wakiwa kwenye mionekano mizuri ambapo wengi wame serve face na makeup zao pamoja na hair styles za kuvutia

Ambacho kinatuvutia kwasasa ni kwamba watu wengi maarufu wamejua umuhimu wa makeup na nywele nzuri kwenye mionekano yao, tunapenda kwamba wanatilia mkazo kwenye hivi vitu.

Leo tupo na wachache ambao tumewaona week iliyopita tukavutiwa na looks zao akiwepo Mwamvita Makamba akiwa kwenye professional photoshoot, ameachia nywele zake akiwa na makeup ambayo ni suitable kwaajili ya professional look, mwingine ambae tumemuona ni Monalisa yeye alikuwa na birthday amefanya photoshoot akiwa ameachia nywele zake vyema na simple makuep look, Rosa Ree a.k.a mama Omoll alikuwa na bob hairstyle akamaliza muonekano wake na bold red lipstick

Lakini kuna ambao wametuonyesha huitaji nywele ndefu kupendeza na makeup yako, unaweza kuwa na nywele fupi na ukapaka makeup vizuri ukapendeza akiwepo mwanadada Feza Kessy akiwa kwenye blonde low cut akiwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa Fezza alichagua simple neat makeup, Jojo Gray kama wedding guest ametuonyesha namna unaweza kurock low cut harusini, akiwa na low black haircut amemalizia muonekano wake na nude makeup huku mwanamitindo jasinta yeye nae akiwa na blonde low cut ametuonyesha unaweza kuwa na a no makeup makeup look na ukapendeza kwenye mizunguko yako ya kawaida

Tuambie muonekano wa nani umependezwa nao zaidi?

Related posts