SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Beauty Na Fashion Tips Za Siku Ya Uchaguzi Mkuu
Urembo

Beauty Na Fashion Tips Za Siku Ya Uchaguzi Mkuu 

Kesho ndio tunaenda kupiga kura na kumchagua Rais wa awamu ijayo, ni matumaini yetu wote mmejiandikisha na mtaenda kukamilisha haki yenu ya kupiga kura. Kama fashion blog tumeona si mbaya tukiwapatia tips chache za nini mvae au kufanya siku hii

  • Vaa Nguo Nyepesi Lakini Sizizo Onyesha Maungo

Yes as tunakuwa tumesimama muda mrefu ni vyema tukavaa nguo nyepesi ili kupata hewa kiurahisi na kutokutoka jasho na kuwakera waliopo karibu yako.

  • Rangi Za Nguo Neutral Na Sizizo Hakisi Jua

Vaa rangi neutral ambazo zio za kichama lakini pia epuka rangi zinazo hakisi jua, maana zinaweza kukupa joto na kukufanya utoke jasho au kushindwa kuvumilia kuendelea kusubiri kwenye foleni ya kupiga kura.

  • Beba Maji

Maji ni muhimu kwenye hili, tunasimama muda mrefu unaweza kupata kiu au kukaukwa na midomo hakikisha umebeba chupa yako ya maji kwa ajili ya hydration

  • Sun Screen Cream

Kama ambavyo tumesema juu mara nyingi vituo vingine hakuna maturubai au miamvuli ya kujikinga na jua hakikisha umepaka sun screen cream yako ili kuepuka jua kuathiri ngozi yako.

  • Vaa Viatu Ambavyo Ni Flat

Epuka struggle ya kuvaa viatu virefu, vaa simple zako nzuri lakini pia hakikisha ni za ngozi na sio za plastic, as we all know plastic juani inaunguza.

  • Deodorant, Body Spray Etc

Hata kama unatoka nyumbani mapema hakikisha umebeba au kupaka hivi vitu, ili kuepuka kutokwa jasho na harufu mbaya ambayo itawakera waliopo karibu na wewe.

Kwa kusema hayo tungependa kuwatakia uchaguzi mwema na wenye amani.

Related posts