Hakika kwetu Afroswagga huwa twafurahi tuonapo watu mbalimbali katika tasnia yetu ya urembo na ubunifu wakikua nakuweza kuleta bidhaa mpya sokoni iwe ni ya nywele, urembo, kucha au hata ngozi.

2018 tumeona baadhi ya bidhaa za urembo zilizoweza fanya vizuri huku tukitaraji kuona zikikuwa na kufikia katika masoko ya kimataifa.

MAKE UP- LAVIE COSMETICS, LASHES

Make-up artist Lavie ameweza launch brand yake ya vipodozi pia lashes na tumeziona zkifanya vizuri. Celebs na hata watu wa kawaida wameweza pendeza with Lavie nasi twampongeza kwa hatua hii, tukitaraji kuona akikwea pia internationally.

@laviemakeup

 

  • NAIL PAINT-LAVY PRODUCTS

Hizi ni rangi za kucha toka kwa mwanamitindo Flaviana Matata ambapo zimeendelea kufanya vizuri sokoni. Katika kuboresha huduma with Lavy Products, wana a nail mobile clinic ambapo mteja hufuatwa alipo akiweka appointment hivyo kuwa manicured au pedicured popote ulipo.

@lavy_products

  • NYWELE- J_ADORE TZ

Katika brands za nywele ambazo zimefanya vizuri basi Mama Jadore ameweza kuwa miongoni mwao. Hudeal na nywele ambapo wig toka J_Adore, hutokoseaga. Pia warembo wetu katika mashindano ya Miss Tanzania tuliona wakipendeza na nywele hizi.

@j_adoreintz

  • BIDHAA ZA MWILI-BEDEE NATURALS

Maarufu kama Mama DD, hutengeneza aina mabalimbali ya bidhaa akitumia vitu asilia kwa ajili ya utunzaji na urembo wa nywele na ngozi ikiwemo mafuta, sabuni, massage oils, face masks na hata kwa ajili ya lishe. Hutumia vitu asilia kama sheabutter, matunda, maua pamoja na miti na huleta mabadiliko kwa mtumiaji.

Comments

comments