Kama mpenzi wa kunukia najua umeshakutana nazo hizi, deodorant, body spray, body mists na perfume ukiyasikia haraka hara haya majina utaona vyote ni sawa lakini kila kimoja wapo kina tofauti na kingine, ikiwa tulishaongelea kuhusu body spray na deodorant leo tunakuleta tofauti ya body mists/splash na perfumes
Body Mists/Splash ni nini?
Body Mists/Splash hazina tofauti sana na body spray zote utengenezaji wake unafanana japo hizi zenyewe ni lighter zaidi kuliko body spray, zinawahi kuisha harufu yake hivyo inabidi u-reapply mara kwa mara lakini pia kuna utofauti katika packaging, ikiwa body spray zinakuwa packed kwenye kopo zisizo unyesha splash au mists zenyewe packaging yake mara nyingi ni transparent na ni plastick japo zipo za udongo.

Perfume zenyewe ni tofauti ikiwa zina high level of oils, alcohol na fragrance hivyo husababisha kuwa na harufu inayokaa muda mrefu lakini pia zina tofautiana katika utengenezaji wake kuna eau de cologne, eau de toillete, eau de parfum, na perfume. Unaweza kujua zaidi kuhusu hizi kwa kusoma click hapa kusoma zaidi – Aina Na Namna Ya Kuchagua Perfume Inayo Kufaa

Tukiendelea na body mists/splash na perfume
Body mist/splash na perfume tofauti zake kubwa ni
- Body Mists/Splash ni lighter na hazikai muda mrefu kwenye mwili wakati perfume ni strong na zinaweza kukaa muda mrefu mwilini
- Body mists/splash unaweza kupaka mwili mzima na isiwe na harufu kali wakati Perfume inashahuriwa upake kwenye pulse point, nyuma ya sikio,shingoni pamoja na nyuma ya magoti.
- Body splash / mists huuzwa bei rahisi zaidi wakati Perfume ni ghali.
Unaweza kufahamu kuhusu Body Spray Vs Deodorant
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…