SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Body Spray Vs Deodorant
Urembo

Body Spray Vs Deodorant 

Inawezekana wewe ni mmoja wapo ambao tunaona body spray na deodorant ni kitu kimoja ukizingatia kwasasa zipo deodorant za kupuliza pia basi tunahisi vyote ni sawa lakini kiukweli kabisa hivi ni vitu viwili tofauti vinatofautiana katika utengenezaji wake, kazi, matumizi pamoja na longetivity zake.

  • Deodorant ni nini?

Ukiachana na kwamba huwa kuna harufu kwenye deodorant lakini kazi yake kubwa ni kuwa clinical agent ambayo ina anti-microbial inayosaidia kupunguza ukuaji wa bakteria ambao husababisha harufu mbaya.

  • Body Spray ni nini?

Body spray mara nyingi hutumika kama m’badala wa perfume, zenyewe zipo tofauti kidogo zina lower lever of concetrated oil & more alcohol, Body spray zina add spritz katika mwili na kufanya unukie fresh bila kuwa na harufu kali kama za perfume.

  • Je Zinatengenezwaje?

Deodorant zinatengenezwa na chumvi pamoja na fragrance ambapo chumvi husaidia kuziba vitobo vinavyo sababisha jasho na fragrance husaidia kupunguza harufu ambayo tayari ipo.

Body Spray hutengenezwa na fragrant essential oils, mafuta haya mara nyingi huwa ya maua, herbs, spice’s na wakati mwingine huwa ni mchanganyiko wa vyote vitatu na huongezewa na alcohol pamoja na pombe ili ku-dilute mchanganyiko ufanye kazi kwa ufanisi.

  • Zinafanyaje kazi?

kama tulivyoelezea hapo juu Deodorant zinakazi ya kuziba vitundu vya jasho kutoa jasho wakati fragrance zilizopo ndani yake zinasaidia kupunguza harufu ambayo tayari ipo,

Body Spray kazi yake ni kukufanya unukie vyema kwa masaa kadhaa, kwakuwa katika utengenezeji wake body spray inatumia maji na alcohol longevity yake sio kubwa sana kama perfume.

  • Unatakiwa Kupaka Wapi?

Deodorant inapakwa makwapani wakati body spray inapakwa kwenye pulse point, nyuma ya masikioni na sehemu nyingine mwilini na hata kwenye nguo.

  • Je unachaguaje utumie kipi?

kazi za hivi viwili ni tofauti kama unataka kupunguza jasho na kunukia kiasi basi tumia deodorant lakini kama unataka tu unukie kiasi na huna tatizo la jasho basi body spray ni chaguo jema zaidi.

Related posts