Si kazi rahisi kwa mtu wa kipato cha chini ku maintain urembo wake, hasa kwa sasa ambapo kila mtu ana taka kuonekana mrembo na bidhaa nazo zina uzwa bei ghali hatari, wakati tunapitia pitia katika blog za wenzetu tukaona hii article ya beauty product zilizo chini ya Tsh 10,000 kutoka kwa http://bintiesque.com, tumeipenda tukaona si mbaya ku share na ninyi pia
1) Katika dressing table yako hutakiwi kukosa mafuta ya nazi haya ni multi functional iwe ngozi, nywele pia yana weza kuwa kama shaving oil. Kwa sasa una weza ukuta mafuta ya nazi yanauzwa hadi elfu 20,000 lakini kumbe yapo ya bei chini yanayo fanya kazi sawa tu na yanayo uzwa bei za juu kuna Parachute ambayo huuzwa kuanzia 8,000/=-5,000/= na pia kuna mafuta ya nazi ya minara ni 1,500/= tsh tu
2)Rose Water ni muhimu pia kwa ngozi na nywele si kitu cha kukosa nyumbani kwako, wengi huwa wana changanya rose water na manjano kwa ajili ya ngozi lakini pia ina weza kutumika kama toner pia katika nywele ni nzuri maji haya yanauzwa 2,500/= tsh tu
3) Excel Paris Lipsticks, hutakiwi kukosa a matte lipstick ambayo ina last 24 hors. Wengi wetu sasa hivi wana kimbilia mac lipsticks ambazo huuzwa kuanzia 10,000 kwenda juu lakini naweza kurecomend hii Excel Lipstick ina kaa muda mrefu na bei yake ni rahisi 1,000 tu kwa moja. nzuri zaidi kama utapaka lip balm kabla hujaipaka yenyewe ili kuipa midomo yako unyevu (kavu sana)
4) kuna make up removals za kila aina na kila bei lakini pia una weza kutumia baby wipes kutolea make up zako, kawaida make up removals zinauzwa kuanzia elfu 10,000 kwenda juu lakini baby wipes kuna mpaka za 2,000.
Kama unavyo vingine vya kushare na sisi ili tuweze kuwasaidia na wengine wasiliana nasi kupitia
Facebook – afroswaggamag
Instagram – afroswagga
Twitter – afroswaggatz
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…