SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

COCONUT AND CASTOR OIL KWA UKUZAJI WA NYWELE
Hair

COCONUT AND CASTOR OIL KWA UKUZAJI WA NYWELE 

Nini kina fanya nywele zikue haraka? wasichana wengi hujiuliza hili swali na hapo ndipo wanapo amua kutafuta majibu kupitia madawa ya salon ambayo ni ghali pia yana kemikali ambazo si nzuri. Kuna mafuta mazuri ya asili ambayo yana weza kukusaidia kukuza nywele zako bila gharama na pia hayana kemikali, leo tuangalie mafuta ya nazi na mafuta ya mnyonyo

Mafuta ya mnyonyo husaidia ku imarisha nywele na kujaza nywele zilizo katika.

Mafuta ya nazi yenyewe husaidia vingi ikiwemo kuondoa mba, kukuza nywele, kuzipa nywele protein na kuzuia ukatikaji wa nywele.

maxresdefault

Kuna njia mbali mbali za kutumia mafuta haya

Castor oil – ili kupaka mafuta haya kata nywele zako katika mafungu mafungu na tumia pamba kupaka mafuta kwenye ngozi kisha zifanyie massage

Coconut oil – una weza kupaka mafuta haya mara mbili kila week kama ilivyo kuwa katika mafuta ya mnyonyo haya pia ukisha paka massage ngozi ya kichwa chako, itasaidia ukuaji wa haraka wa nywele.

Lakini pia unaweza kutumia mafuta haya Kama hair mask kwa kufanya hivi

Mahitaji

  • Vijiko Vitano vya mafuta ya nazi
  • Vijiko vitano vya mafuta ya mnyonyo

changanya mafuta hayo kisha paka kwenye ngozi ya kichwa bila kusambaza kwenye nywele, baada ya kupaka kichwa chote fanyia massage kichwa chako kwa dakika tano kisha sambaza kwenye nywele vaa kofia ya plastic na funga taulo kwa masaa mawili japo ukikaa nayo usiku mzima itapendeza zaidi, Kisha osha na fanya conditioning yako kama kawaida una weza kufanya hivi mara mbili au moja kwa mwezi, ukifanya inavyo takiwa utapata matokeo mazuri si tu nywele kukua bali zitakua na afya na kung’aa

Related posts