SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

COSRX Advanced Snail 92 All in One Cream Review
Reviews

COSRX Advanced Snail 92 All in One Cream Review 

Moja kati ya product ambazo zina hype sana huko mtandaoni iwe tiktok, instagram etc ni hii COSRX Advanced Snail 92 All in One, beauty influencers wengi wameonekana kuiongelea na kupendekeza wengine watumie, leo tupo hapa kukupa review yake.

Kwanza abisa unahitaji kujua hii product inatengenezwa kutoka Korea (K Beauty Product) na ipo kwa miaka mingi, kwasasa imekuwa hyped kutokana na mitandao as we all know kampuni zinatumia influencers kwa wingi kutumia product zao na ziongelewe mitandaoni.

Kama ambavyo jina linasema product hii imetengenezwa na 92% ya snail slime / mucin ( hii ni ule ute unaotoka kwa konokono) huu ute unaaminika kuwa mzuri katika ngozi hasa kwenye kupunguza makunyanzi, kurepair ngozi zilizo haribika, kuondoa madoa na alama za chunusi.

Ukiachana na snail lime / mucin product hii ina Hyraronic Acid ambayo nayo ni nzuri kwa kufanya skin stretch & flex na kupunguza mikunjo ya ngozi.

Je Product hii inasaidia nini?

kama tulivyodadavua kuhusu ingredients zilizopo kwenye product ya COSRX Advanced Snail 92 All in One hii product inasaidia

  • Kuipa ngozi yako unyevu
  • Inasaidia kurekebisha na kutuliza ngozi iliyoharibika
  • Husaidia kufufua na kuifanya ngozi kuwa na mng’ao bora
  • Hutoa collagen kwa uboreshaji wa elasticity ya ngozi na faida zingine za kuzuia kuzeeka

Inafaa kutumika na mwenye aina gani ya ngozi?

  • Japo bidhaa hii inasemekana kufanya kazi kwa kila aina ya ngozi hii product ni nzuri zaidi kwa wenye combination na oily skin.

Unaitumiaje?

  • Ukishamaliza kuosha uso na kupaka toner, chukua cream yako na upake kwenye uso kisha subiri dakika kadhaa ili iweze ku-absorb ndio upake sun screen na makeup (kama ni mtu mwenye haraka asubuhi basi haifai bora uitumie usiku kwa maana inabidi usubiri kidogo ikauke kabla ya kuendelea na step nyingine)

Harufu

  • Cream hii haina harufu kali kwa sababu ni alcohol & fregance free, na kwasababu hii pia inafaa kwa sensitive skin.

Texture

  • Hii product ina teleza sio kama cream nyingine, inaweza kuteleza kwenye vidole kabla haijafika usoni, ni vyema kuitumia kwa uangalifu na haraka kama unaujua ute wa konokono basi utajua kwanini inateleza.

Inafaa kwa msimu gani?

  • Hii product ni nyepesi kwaio inafaa kupakwa majira ya joto, incase ni majira ya baridi itakubidi upake layers mbili adi tatu.

Kwanini Inapendwa?

Spreadable Inapakika vizuri usoni

  • Light weight, sio nzito ni nzuri kwa majira yetu ya Africa
  • Hydrating inaweka unyevu katika ngozi
  • Gentle as haina chemicals nyingi si rahisi kupata reaction unless uwe na alergy na moja ya kemikali zilizopo

Expiry

  • Inatakiwa utumie ndani ya miezi 12, kama itazidi hapo inakuwa ime haribika.

Bei & Upatikanaji

  • Bei zinauzwa kati ya 45,000 mpaka 60,000/
  • Zinapatikana katika maduka ya urembo hasa wanayouza bidhaa za Kikorea

Hayo ndio maoni yetu katika bidhaa hii lakini hakikisha kabla ya kuitumia unapata ushauri kwa specialist wa ngozi na pia jaribu kidogo kidogo kabla hujaanza kuitumia kila siku as we all know kila product ina reaction tofauti katika kila ngozi.

Related posts