Kama ni mmoja ya wapenda accessories basi utakuwa umeshakutana nazo nyingi sasa hivi hizi bracelets au mikufu na pete zina-trend sana. Tunakutana nazo kwenye maduka mbalimbali huku bei zake zikiwa za kuridhisha lakini Je unajua kwamba hizi accerries original yake ni kutoka katika brand kubwa ya vito kutoka ufaransa?
Kutoka mwaka 1906 Van Cleef & Arpels wamekuwa wakitengeneza vito ambavyo vilisimama kama lucky, joy & optimism japo mwaka 1968 ndipo hii four leafe clover ndipo ilipokuwa introduced na brand hii ikipewa jina la Alhambra collection

Kwa wale ambao hatujui Four Leaf Clover ina maanisha faith, hope,love & lucky. Wakati wanaanza walianza na mikufu lakini wakaanza kutengeneza na bangili, hereni, pete na pendants. Watu maarufu mbalimbali wameonekana kuvalia vito hivi akipewepo Catherine, princess of the Wales.

Genuine Van Cleef & Arpels inatengenzwa kwa kutumia 18k yellow, white au rose gold. Well hivi karibuni tumemuona mwanamuziki kutoka Nigeria akiwa amevalia ya kwake,


ambapo tumezoea kuziona nyingi zikiwa na rangi moja iwe gold white, green au nyeusi ya kwake imeonekana kuwa na rangi tofauti tofauti ambazo zina Diamond, Mother-of-pearl.

Ommy Dimpoz yeye ameonekana nazo mbili nyeusi na nyekundu ambayo nyekundu ina yellow gold, Carnelian huku nyeusi ni yellow gold, Onyx

Bangili hizi zinaanza kuuzwa kwa Usd 5300 sawa na Tsh 13,311,750.30/-
Note: Inasemekana vito hivi vipo very delicate vinachunika kwa haraka,ni vyema usivae na accessories nyingine, usioge wala kupaka perfume ukiwa umeviavaa
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…