SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Dhambi Za Ngozi Unazotakiwa Kuziacha
Urembo

Dhambi Za Ngozi Unazotakiwa Kuziacha 

Inawezekana unajua na inawezekana haujui kama unachofanya ni dhambi katika ngozi yako na unatakiwa uache kukifanya kwasababu inaweza kuwa ni sababu ya ngozi yako kuharibika

 • Kukaa Sana Juani Bila Ya Kupaka Sun Screen

sunscreen ni nini?  Sun screen ni lotion au cream ambayo imetengenezwa kulinda ngozi na jua, na sio tu ukiwa juani bali inashauriwa kupakwa hata kama haupo juani, Inafaida nyingi ikiwepo Kutokupata mikunyanzi ya uzee, kuondoa / kutopata madoa usoni lakini pia kukuepusha na maradhi ya cancer

Umuhimu Wa Kupaka Sunscreen Katika Ngozi

 • Kutokunywa Maji Ya Kutosha

Maji yanafaida mbali mbali katika ngozi na ni moja ya dawa kubwa ya kuwa na ngozi nzuri na yenye afya hufanya ngozi kung’aa kwa kuwa na afya, pia kupungua/ kumaliza chunusi maana viwango vya maji na mafuta kwenye ngozi vinakuwa katika uwiano. Hydration is the key inashauriwa kunywa litre mbili za maji kwa siku. Hii sio tu inasaidia kwenye ngozi lakini pia katika afya ya mwili wako

Tiba ya Maji Kwa Afya Yako

 • Kuosha Uso Haraka

Wote huwa tumechoka hasa wakati wa usiku umesha choka na kazi yet unatakiwa ufanye skin care routine ya usiku basi unanawa tu harakaharaka umalize upate kupumzika, hii ni dhambi kwa maana unaweza ukanawa na uso ukawa haujasafishika. Chukua muda wako kuuosha taratibu na pitisha sabuni kila mahali, hakikisha unaosha uso wako si chini ya mara mbili lakini pia usizidishe.

 • Kupata Ushauri Wa Vipodozi Kupitia Rafiki Yako

Katika vitu ambavyo vinatu-cost wengi ni kuuliza kwa marafiki utumie kipodozi gani, au kwa sababu ngozi ya rafiki yako nzuri unamuuliza anapaka nini na wewe ukapake, hii ni dhambi kubwa ya ngozi. Kwa sababu wote hatuna ngozi sawa kinachomfaa yeye kinaweza kisikufae wewe na kinaweza kuharibu kabisa ngozi yako. Hakikisha unaenda kwa wataalamu wa ngozi kwa ushauri bora

Unatumia kipodozi gani?

 • Kutokusafisha Vifaa Vyako

chochote ambacho kinagusa ngozi yako ya uso kinatakiwa kisafishwe mara kwa mara, kama simu, makeup brushes, taulo, mashuka pamoja na foronya zake. Kwenye hivi vitu kunaweka kuwa na dead skin cells na bacteria zilizo jitengeneza, lakini sio tu hivyo mikono yetu nayo inatakiwa kuoshwa mara kwa mara ikiwa tunagusa na kushika vitu mbalimbali kisha tunashika nyuso zetu bila kujua inaweza kutuletea madhara.

Sababu 3 Muhimu Za Kwanini Usafishe Makeup Brushes Zako

Afromates tuambie wewe ni dhambi gani una commit mara kwa mara lakini pia kuna muendelezo utakao kuja hivi karibuni

Related posts

3 Comments

 1. psychedelic mushroom chocolate bars legal near north carolina

  … [Trackback]

  […] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/dhambi-za-ngozi-unazotakiwa-kuziacha/ […]

 2. 3 musketeers (chocolate bar)

  … [Trackback]

  […] There you can find 81413 more Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/dhambi-za-ngozi-unazotakiwa-kuziacha/ […]

 3. buy 4-aco-dmt online quality,

  … [Trackback]

  […] There you will find 63320 more Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/dhambi-za-ngozi-unazotakiwa-kuziacha/ […]

Comments are closed.