SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Do & Dont’s Wearing Jewelry At The Office
Urembo

Do & Dont’s Wearing Jewelry At The Office 

Mavazi ya ofisini yanaweza kuwa boring hasa kwa wale ambao wanavaa sare ofisini au ambao bado hatujajua namna ya kufanya mavazi hayo yawe stylish na yet yawe kiofisi zaidi, mara nyingi huwa tunakimbilia kwenye jewelry ambazo tunajua huwa zinaiunua vazi, lakini huwa tunakosea kwa kuvaa jewelry ambazo haziendani na sehemu husika.

Tuko hapa kukupa tips chache za Do & Dont’s wearing jewelry at the office

  • Chagua Jewelry zinazoendana na mwili wako

Sababu kubwa accessories ni muhimu ni ku-control muonekano wako hasa kuondoa attention sehemu ambayo haitakiwi kuwa na attention, hivyo ni vyema kuchagua jewelry ambazo zinaendana na wewe na kuku-compliment bila ya kuweka attention kubwa isiyotakiwa.

Mfano Mikufu mirefu ni mizuri endapo unataka kufanya shingo yako ionekane ndefu, ila inaweza kuwa distraction endapo utavalia mkufu na vazi ambalo linaonyesha kifua hii itasababisha macho yote yawe kifuani, hakikisha unachovaa kinaendana na wewe na sehemu husika.

  • Usivae Jewelry zinazo ng’aa sana au rangi kali

Tunajua tunapenda ku-match mavazi yetu na vito vyetu lakini kuna sehemu husika za kufanya hivyo, una mitoko nje unaweza kuvaa ofisini huitaji kung’aa sana, vaa zile zenye design na rangi zilizo calm.

  • Limit Your Statement Pieces

Ni kweli statement jewelry zinanyanyua muonekano lakini kwa ofisini huitaji kuwa too bold, unaweza kuchagua kimoja kiwe statement wakati vingine vikiwa kawaida mfano unaweza kuvaa hereni statement huku kwingine kukiwa simple kama saa au mkufu.

  • Usivae Jewelry Zinazopiga Kelele

Una tembea kutoka huko wafanyakazi wenzio wanasikia kelele za bangili au mikufu yako, vaa jewelry ambazo hazina kelele ilikuepuka kuleta usumbufu kwa wengine.

Tukutakie week njema.

Related posts