SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Do & Dont’s Of Wearing Perfume At Work
Urembo

Do & Dont’s Of Wearing Perfume At Work 

Perfume can be the cherry on top when it comes to represent ourselves hii ni kama itatumika vyema lakini kama itatumika vibaya unaweza kuwa labelled kama perfume offender, sote tunapenda kunukia vyema popote tulipo lakini kuna sehemu zinafaa kuwa na perfume za aina fulani mfano mzuri ni kazini / ofisini.

  • Je Perfume Zinaruhusiwa Kazini

Inategemea na sehemu unayofanya kazi kuna ambao wanaruhusu na ambao hawaruhusu kutokana na sababu mbalimbali, na perfume hupakwa kutokana na sehemu unayofanya kazi mfano kama unafanya kazi kwenye vituo vya afya mara nyingi unashauriwa kutokutumia manukato, kama ni office /retail inashauriwa kutumia manukato sahihi na kama ni kazi za nje basi hapa mara nyingi unaweza kutumia manukato yoyote.

Kazi yoyote ambayo utakuwa unafanya ni vyema ukajua nguvu ya perfume kwa mazingira yanayo kuzunguka, hizi ni tips chache za nini ufanye na nini usifanye kutumia manukato ofisini,

  • Chagua Manukato Yasiyo Nukia Sana

Unapokuwa ofisini hakikisha unatumia light scents, wenyewe tunaita harufu za kizungu hakikisha unanukia lakini sio mpaka unawakera wengine, manukato yako yawe ambayo yananukia kiasi.

Aina Na Namna Ya Kuchagua Perfume Inayo Kufaa

  • Less Is More

Unapokuwa ofisini hakikisha unapulizia manukato yako kwa kiasi,na ili yadumu muda mrefu basi pulizia zile sehemu ambazo zinafanya manukato yakae muda mrefu kama shingoni, nyuma ya masikio na kwenye wrist (kiganja)

Sehemu Za Kupuliza Unyunyu “perfume” Idumu Kwa Muda Mrefu

  • Wafikirie Wengine

since ofisini kuna watu wengi na unakaa masaa mengi zaidi ni vyema ukawafikiria na wengine, kuna ambao wana allergies au wako sensitive na manukato unaweza kuwa unawaumiza au kuwakera basi hakikisha unapaka manukato ambayo yatakuwa sawa na wengine.

  • Usipake Au Ku-Reapply Perfume Ofisini

Uko ofisini na wengine unatoa perfume yako kwenye pochi unaanza kujipulizia au imefika mida ya mchana unaenda chooni una-reapply perfume hii ni nzuri kama una perfume ambayo hainukii sana ila kama inatumia muda kupoa then hakikisha ukijipulizia asubuhi imetosha usiende kukera wengine tena.

Related posts