Weekends wengi tunapenda kwenda kujifanyia treatment za urembo kama kuosha na kusuka nywele, kwenda spa kwa ajili ya massage na matibabu ya ngozi hasa usoni. Lakini vipi kama huna pesa au unasikia uvivu kwenda Spa siku hio? haimaanishi usifanye vyote hivi unaweza kujifanyia vyote mwenyewe nyumbani tena basi kwa vitu ambavyo unavyo tayari.
Step 1: Ondoa Makeup Na Usafishe Uso
Kabla ya kufanya lolote kwanza kama ulikuwa na makeup usoni kwako inabidi uondoe, ili kuwezesha ngozi kupata treatment ipasavyo, inategemea na wewe uwa unafanyaje katika kuondoa makeup yako unaweza kutumia makeup remover au kienyeji kwa kutumia mafuta ya nazi
Namna ya kutumia mafuta ya nazi kuondoa makeup
- Chukua pamba itumbukize katika mafuta yako ya nazi
- ukisha ridhika na kiwango cha mafuta katika pamba toa na uanze kufuta uso wako taratibu
- utaona makeup inaondoka futa yote kadri uwezavtyo.
Safisha Uso.
Ili kujiandaa kwa ajili ya facial ni lazima usafishe uso wako vizuri kabisa kwa sabuni ili kuondoa mafuta ya nazi au make up remover au unaweza kutumia pia cleanser au asali
Namna ya kutumia Asali kusafisha uso
- Hakikisha umesha osha uso wako vizuri
- chukua kijiko kimoja cha asali na uanze kupaka usoni
- sugua taratibu kwa dakika 5 ili upate kuondoa ngozi zilizo kufa lakini pia kuzibua vitobo vya ngozi vilivyo ziba.
Step 2: Steam/Mvuke
- Chukua nguo safi ( preferably towel /taulo) weka katika maji ya vuguvugu likaushe kidogo na uweke usoni
- pia unaweza kuchemsha maji ukaweka kwenye beseni au bakuli kubwa na kuliinamia upate mvuke.
- kama una mafuta ya rose mary unaweza kuyaongezea ili kuongeza mchakato wa utakaso (cleansing process.)
- steam uso wako kwa dakika 10-15 usizidishe.
- kama una sensitive skin skip hii process inaweza kusababisha matatizo
Step 3 : Mask
- hapa inabidi ujue aina ya ngozi yako na mask gani unatakiwa utumie.
- kwa wenye ngozi za mafuta unaweza kujaribu mud au clay mask ili kunyonya mafuta katika ngozi yako
- kwa ngozi kavu hapa itabidi utumie mask ambazo zinasaidia kuongeza maji na mafuta katika ngozi yako
- paka mask yako kwa dakika 15 na uoshe uso wako na kuukausha.
- unaweza kutumia natural mask au read made mask za kununua madukani
Step 4 : Paka mafuta
ili kuilanisha ngozi yako na kuifanya ipendeze paka mafuta katika ngozi mara baada ya kumaliza hizi process zote, kisha baada ya hapo enjoy your glowing skin.
Related posts
3 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/do-spa-like-facials-at-home/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/do-spa-like-facials-at-home/ […]
… [Trackback]
[…] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/do-spa-like-facials-at-home/ […]