SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Does Your Skin Break Out Before It Clears Up?
Urembo

Does Your Skin Break Out Before It Clears Up? 

Umeshawahi kuanza kupaka kipodozi kisha ngozi yako ikaharibika zaidi ya ilivyokuwa mwanzo? Yes hii huwa inatokea na mara nyingi wengi wetu huwa tunachukulia hii kama dalili ya kipodozi kutokutupenda au ku-fail.

Leo tunakuletea au kukufahamisha juu ya Skin Purging, Skin Purging hii ni pale unapoanza kutumia product mpya za ngozi na ukaanza kuona ngozi yako inazidi kuharibika, hii ni process ya ngozi kusafishwa ambapo ngozi inajiondoa yenyewe ya mafuta, bakteria, au uchafu na ndipo unapoona chunusi zinatokea kuliko kawaida lakini kitu kizuri juu ya Skin Purging ni kwamba haikai muda mrefu huchukua week chache na zinapotea.

Lakini pia haimaanishi kila mtu ataona skin purging, hii hali hutegemea na ngozi ya mtu wengine zinaweza kusafishika tu bila ya kuharibika wakati wengine wanapitia skin purging na pia inategemea na ukubwa wa tatizo lako ndani ya ngozi ambacho kinatakiwa kutolewa nje ili kupata ile ngozi unayoitaka.

Jambo lingine la kuzingatia: Wakati wa utakaso (Skin Purging) baada ya kuanza utaratibu mpya wa kutunza ngozi au baada ya kutumia vipodozi vipya, chunusi ambazo ni ndogo huwa hazionekani kwa jicho la kawaida zinaanza kutoka chini na kuja juu ya ngozi sehemu ambazo uhathirika zaidi na skin purging ni kwenye paji la uso, kidevu pamoja na sehemu za puani kutokana na kwamba hizi sehemu huwa na mafuta mengi.

Je utajuaje kama ni Skin Purging au Kipodozi hakija kupenda?

Skin Purging haikai muda mrefu lakini pia hutokea sehemu ambazo tayari zimeathirika mfano kama ulikuwa na chunusi kwenye paji la uso basi utaona zinazidi kutokea sehemu hio

Kipodozi Kutokukupenda huwa inatokea sehemu nyingine mbali na zile ambazo unatatizo lakini pia huchukua muda mrefu kupotea zaidi ya week sita.

Nini Cha Kufanya Endapo Ngozi Yako Inapitia Kipindi Cha Skin Purging

Unatakiwa kuendelea na routine yako kama kawaida na hakikisha upo consistent nayo bila ya kuacha, lakinipia huchukua week nne mpaka sita kuona matokeo unatakiwa kuwa mvumilivu.

Ni matumaini yetu umejifunza kitu.

Related posts