SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Dondoo 7 Za Kutunza Ngozi Yako Wakati Huu Wa Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani
Skin Care

Dondoo 7 Za Kutunza Ngozi Yako Wakati Huu Wa Mwezi Mtukufu Wa Ramadhani 

Ramadhani ni ibadah ambayo inatekelezwa na waislamu wote Duniani, kwenye ibadah hio ambayo inahusisha kujizuia kula na kunywa pamoja na mengineyo. Inaweza kukupa wakati mgumu ngozi yako kuonekana bora kwa wakati huu. Hizi ni Dondoo 7 za kufanya wakati huu wa Ramadhan ili ubaki na ngozi yenye Afya.


1. Maji Maji Maji Kukosa kunywa maji kwa masaa inaweza kusababisha ukavu kwenye ngozi yako, hivyo basi wakati wa kufuturu unapofika hakikisha unachukua kiwango stahiki cha maji. Na vimiminika vya kutosha. Vile vile unaweza kunywa maji ya kutosha wakati wa kula Daku. Maji haya yataendelea kutumika siku nzima hadi wakati wa kufuturu unapofika tena.


2. Epuka kunywa kahawa na vinywaji vya kikaboniki ( soda, carbonated drinks). Kahawa inajulikana kama Diuretic drink yaani kinywaji chenye sifa ya kusababisha kukauka maji mwilini, wakati huu wa Ramadhan unahitaji maji ili ngozi yako iendelee kubaki na unyevu wa kutosha.


3. Paka mafuta stahiki kulingana na mahitaji ya ngozi yako. Wakati huu ambao wengi mpo nyumbani ama unatumia muda mwingi nyumbani hivyo unakosa kuona umuhimu wa kuendelea ku moisturize ngozi yako. Lakini wakati  huu ambao na Ramadhan imetujia endelea kumoisturize yako ili iendelee kubaki na unyevu na kuwa na afya njema.


4.  Kula zaidi matunda, mboga mboga, vyakula vya nyuzi nyuzi “fibers”. Makundi haya ya Chakula yanasifa nzuri ya kuimarisha afya ya mlaji na hivyo ngozi yako itaendelea kuwa na afya njema.


5. Epuka bidhaa za maziwa ” Diary Products”. Bidhaa hizi zinasifika kwa kusababisha ongezeko la chunusi, hutopenda kuona chunusi zinazidi wakati huu wa Ramadhan ikizingatiwa inafatiwa na Eid. Wakati huu epuka maziwa, mtindi na Jibini ili ngozi yako ibaki salama.


6. Linda na Tunza macho yako. Ngozi ya jicho ni laini zaidi. Ina uwezo wa kupoteza unyevu kirahisi na hivo ni vyema kutumia eye cream au eye gel zinazopatikana kwenye maduka tofauti tofauti ya vipodozi na urembo.
Pia unaweza kuandaa tango na kuweka machoni kwa kufanya  ifuatavyo:

  • Chukua Tango lako, lioshe vizuri, kata vipande vya duara kisha weka machoni baada ya dakika 20 osha na maji ya kawaida. Kisha paka eye cream / eye gel yako. ( kama hauna tango pekee linaweza kukusaidia )
  • Fanya hivyo hadi upate matokeo unayoyapenda.

7. Lala usingizi wa kutosha. Wakati wa Ramadhan ni muda wa kuzidisha maombi zaidi na kupumzika vizuri sana. Endelea kulala vya kutosha kwa ajili ya ngozi yako na afya yako kwa ujumla.

Ramadhan Mubarak! ©️binturembo

Related posts

1 Comment

  1. pop over here

    … [Trackback]

    […] Find More Info here on that Topic: afroswagga.com/urembo/dondoo-7-za-kutunza-ngozi-yako-wakati-huu-wa-mwezi-mtukufu-wa-ramadhani/ […]

Comments are closed.