Facial Cleanser ni kitu kinacho safisha ngozi ya uso kutokana na uchafu usoni kama make up, mafuta,cells za ngozi zilizo kufa, vumbi na chochote kile kisicho takiwa usoni, hii husaidia kupunguza matatizo ya ngozi kama chunusi pia kufungua mashimo yaliyo zibwa na uchafu.
Kwa sasa watu wengi hununua cleanser na chache ni nzuri ila nyingi ni mbaya una weza kupata ina uma ukisafishia au hata kuwasha na kuleta vipele usoni leo tuna kuletea facial cleanser ambazo unazo nyumbani lakini hukuwa unajua kama zina faa, mara nyingi facial cleanser hutumika jioni baada ya mihangaiko kabla au baada ya kuoga.
Mafuta ya nazi
mafuta ya nazi si ya kuacha kuwa nayo nyumbani kwako yanakazi nyingi ki afya ya mwili, ngozi na nywele pia. Unacho takiwa kufanya baada ya mizunguko na una taka kusafisha uso wako chukua kiasi cha mafuta mkononi mwako, kisha paka usoni fanyia massage uso wako kwa dk 30 kisha chukua taulo weka kwenye maji ya uvuguvu na uliweke usoni kisha futa mafuta hayo, cleanser hii ina tumika na mtu mwenye ngozi ya aina yoyote si tu inasafisha ngozi bali pia ina moisturize ngozi yako na kuondoa makunyanzi ya uzee usoni.
2)Apple Cider Vinegar Face Cleanser
Apple Cider Vinegar nayo si ya kukosa nyumbani kwako unacho takiwa kufanya ni kuchukua apple cider vinegar kwenye bakuli, chukua pamba na uanze kupaka usoni (kwa mtindo wa ku dab) kisha kama kwa mafuta ya nazi chukua taulo weka katika maji ya uvugu vugu na ufute uso wako, hii husaidia kuondoa mikunjo usoni.
3)Asali na Limao Facial clearance
Kabla ya kupaka facial cleanser yoyote kwanza chemsha maji weka katika beseni na uinamie mvuke kwa dk kadhaa ili kusaidia kufungua vitobo vya vinyweleo vilivyo zibika kisha, chukua vijiko viwili vya asali na kijiko kimoja cha maji ya limao changanya na upake usoni na shingoni acha mkapa ikauke kisha ondoa kwa kuosha uso hii husaidia kuondoa vipele kutokana na limao na ku moisturize ngozi kutokana na asali
kama una swali ama maoni tafadhali tuachie katika kurasa zetu za mitandao ya kijamii
Instagram – afroswagga
Twitter – Afroswaggatz
Facebook -Afroswaggamag
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…