kwa kutumia vitu vichache kutoka jikoni, una weza kutengeneza na kupata face scrubs bila kuwa na wasiwasi wa kupata madhara kutokana na makemikali, kutumia kitu ulicho tengeneza mwenyewe kuna kupa nafasi nzuri ya wewe kuondokana na kuingiza makemikali katika ngozi yako.
Tutakupa njia tatu na rahisi za kutengeneza facial scrub kutoka nyumbani na tuta focus katika vitu vitatu
- Cleansing – kuonda make up, kusafisha mafuta, kukaza ngozi ya uso na kuondoa ngozi zilizo kufa (dead skin)
- Moisturizing – kuipa ngozi unyevu
- Exfoliating – Kusafisha na kuondoa ngozi zilizo kufa
Namna ya kufanya
- Cleansing – process hii ina kusaidia kuondoa makeup, kutoa mafuta na kuondoa ngozi zilizo kufa hapa ina saidia kukinga ngozi yako dhidi ya chunusi (vipele) na kufungua vishimo vilivyo zibwa. una hitaji vitu vitatu, a) oatmeal (ngano nzima) b) Asali 3) mtindi
Chukua kijiko kimoja moja cha hivyo vitu vitatu vyote ( ngano nzima, asali na mtindi)
changanya hivyo vyote katika bakuli na anza kupaka kwa mtindo wa duara kuanzia kwenye kidovu mpaka kwenye komwe (forehead) kaa nayo kwa muda wa dakika mbili kisha futa kwa maji ya uvugu vugu ukimaliza osha tena kwa maji ya baridi ili kufunga vitobo na futa kwa taulo safi.
- Moisturizing – ili kuipa ngozi yako unyevu na isiwe kavu sana una takiwa kuwa na vitu vitatu a) limao b) baking soda c) asali
changanya kijiko kimoja kimoja cha sali, limao na baking soda anza kupaka kwa mtindo wa duara kuanzia kwenye kidovu mpaka kwenye komwe (forehead) kaa nayo kwa muda wa dakika mbili kisha futa kwa maji ya uvugu vugu na futa kwa taulo safi.
- Exfoliating– ili kupata ngozi nyororo na yenye ung’avu tumia sukari ya brown, olive oil na asali
chukua kijiko kimoja kimoja cha asali,olive oil na sukari ya brown changanya anza kupaka kwa mtindo wa duara kuanzia kwenye kidovu mpaka kwenye komwe (forehead) kaa nayo kwa muda wa dakika mbili kisha futa kwa maji ya uvugu vugu na futa kwa taulo safi.
Related posts
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…