Je, umewahi kusikia kuhusu blacksoap? Naongelea African blacksoap,
African Black Black ni sabuni iliyotengenezwa na majivu ya mimea kama vile mboga za kakao, majani ya mitende na mti wa shea. Sabuni hii hutengenezwa Afrika Magharibi, kawaida Ghana.
Sabuni hii hutakasa ngozi vizuri sana hivyo ni nzuri kwa watu wenye matatizo mbalimbali ya ngozi. Sabuni ina uwezo wa kuua bacteria kwenye ngozi hivyo inaweza kusaidia kutibu chunusi. Watu wengine hutumia sabuni kama shampoo au makeup remover.
Ikiwa unajaribu kupunguza kiasi cha sumu unazoweka kwenye ngozi yako, African black soap hupunguza uchafu bila kemikali hatari. Tafiti chache zimefanyika juu ya african black soap lakini utafiti uliopatikana umeonyesha kwamba sabuni hii ina uwezo wa kupambana na bakteria ambayo inasaidia kutibu hali mbalimbali za ngozi.Baadhi ya matumizi ya sabuni hii ni:
Baadhi ya matumizi ya sabuni hii ni:
- kupambana na chunusi
- kuwa na rangi moja
- kuondoa madoa ya chunusi usoni
- kupunguza tango tango
- Pumu ya ngozi

Namna Ya Kutumia African Black Soap Kutatua Matatizo Mbalimbali:
- kupambana na chunusi
Osha uso wako Kwa kutumia African black soap asubuhi na kabla ya kulala, African black soap ina lauric acid ambayo hupatikana katika coconut oil na palm kernel oil ambazo hutumika kutengenezea African black soap zinasaidia katika kupambana na chunusi.
- kuwa na rangi moja
Mafuta yanayopatikana katika sabuni hii yanasifika kuwa na Vitamin A na E ambazo husifika katika kutakatisha na kusafisha ngozi, kama utaogea au kutumia hii sabuni basi utakuwa na rangi moja mwili mzima.
- kuondoa madoa ya chunusi usoni
Kama una madoa ya chunusi, stretch marks, makovu basi African black soap ni jibu lako, sabuni hii ina shea butter ndani yake ambayo husifiwa kwa kuwa na uwezo wa kungarisha ngozi, tumia sabuni hii kuogea au kuoshea sehemu zilizo athirika mara mbili kwa siku kupata matokeo kwa haraka.
- Pumu Ya Ngozi
Viungo vilivyopo katika African black soap vinauwezo wa kutuliza na kupunguza Pumu ya ngozi, badala ya kutumia vipodozi vyenye kemikali vyema bora utumie African black soap utapata matokeo mazuri lakini bila kuharibika ngozi yako
- Ukweli kuhusu african blacksoap!
Ni sabuni nzuri bei yake nzuri na pia ina uwezo wa kutibu chunusi zako ikiwa tu utaitumia kama inavyopaswa. ( vizuri zaidi ukawasiliana na muuzaji atakupa maelezo ya kutosha Kutokana na kwamba utengenezaji hutofautiana)
- Kingine muhimu ni kuendelea na hatua zingine za kutunza ngozi yako kwa sababu kuosha uso pekee pasipo kufuata zingine muhimu bado hujatatua tatizo!
Jee umewahi kutumia African Black Soap, shea na sisi experience yako!
Related posts
2 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-african-black-soap/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-african-black-soap/ […]