SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Fahamu Zaidi Kuhusu Microblading Eye Brows
Urembo

Fahamu Zaidi Kuhusu Microblading Eye Brows 

 • Microblading ni nini?

Microblading ni cosmetic procedure ambayo huingiza rangi chini ya ngozi yako ya nyusi kwa kutumia sindano au mashine ya umeme na sindano. Microblading inakusudia kukupa well-defined eyebrows (nyusi) zilizoainishwa vizuri na kuonekana maridadi, procedure hii inasaidia kupunguza kuwa unapaka wanja kila siku, kwa maana rangi hii hukaa muda mrefu. Inawezakana kukaa kwa miezi 18-30.

 • Imeanzishwa lini?

Procedure hii si mpya imekuwepo kwa takribani miaka 25 huko Asia na imekuwa ikitumika na maarufu nchini Merika na Ulaya, ndio maana unaweza kuona mtu maarufu kaamka na nyusi zake zimetindwa vyema tu.

 • Je Hukaa Kwa Muda Gani?

Lakini rangi hii hupotea kama ambavyo tumesema inaweza kukaa kwa muda mrefu lakini pia inategemea na aina ya ngozi yako, kwa inavyosemekana, ukiwa na ngozi yenye mafuta sana inaweza isikae kwa muda mrefu kama wale ambao wanangozi kavu au mchanganyiko. Kiwango kikubwa cha sebum, au mafuta, yanayofichwa ndani ya ngozi yako inaweza kufanya iwe ngumu zaidi kwa rangi hii kukaa kwenye ngozi yako kwa muda mrefu.

 • Ongea na mtaalam wako juu ya wasiwasi wowote ulio nao juu ya aina yako ya ngozi na ni muda gani unaweza kutarajia matokeo yako yatadumu.
Picture By @glammadam
 • Inachukua Muda Gani Kupona?

Microblading inachukua siku 10 hadi 14 kupona na rangi kukaa katika umbo lake. Wakati wa mchakato huu, ngozi yako ya nyusi itakuwa sensitive, inakuwa laini na nyekundu kutokana na sindano kupita maeneo hayo.

Wakati mchakato wa kupona unaendelea usikune wala kushika kwenye eneo husika, endapo utafanya hivyo unaweza kusababisha vijidudu ambavyo vinaweza kunaswa chini ya ngozi yako na kusababisha maambukizo

Katika kipindi hiki cha uponyaji, unapaswa kuepuka kila aina ya unyevu kwenye nyusi zako. Hii ni pamoja na jasho kupindukia kutokana na kufanya kazi au kwa kuziloesha wakati unaoga bafuni au kwenye pool, kwa kifupi keep away any unyevu kwenye eneo hilo.

 • Tahadhari na hatari

Kama unafikiria kufanya microblading, unapaswa kuzingatia hatari kadhaa:

Ukifanya Microblading tu, nyusi zako zitakuwa na rangi na umbo sawa hadi rangi iishe ( Kama ambavyo tulikua tunaona nyusi za Munah Love japo yeye alifanya tattoo) – ambayo inaweza kuchukua miezi 18 au zaidi. Kuwa na mashauriano ya kina na mtaalamu wako ambayo ni pamoja na kupitia jalada lao na kuwa na mchoro wa sura ya majaribio kwenye uso wako ili uweze kukagua namna utakavyokuwa kwa kipindi kirefu, yes miezi 30 ni sawa na miaka miwili na nusu.

Kutokana na kutumia sindano kufanya procedure hii unaweza kupata maumivu kwenye nyusi na endapo hutokuwa muangalifu kuweka eneo la nyusi safi na kavu basi unaweza kupata maambukizi ya sepsis na athari nyingine.

Note: kama unafikiria kufanya microblading, ni muhimu kufanya utafiti wako na kupata mtaalamu aliye na leseni, aliyekaguliwa vizuri, na anayeaminika

Related posts

3 Comments

 1. check over here

  … [Trackback]

  […] Find More Info here on that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-microblading-eye-brows/ […]

 2. ufabet365

  … [Trackback]

  […] Find More on to that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-microblading-eye-brows/ […]

 3. mushroom shop Portland

  … [Trackback]

  […] There you can find 94636 more Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-microblading-eye-brows/ […]

Comments are closed.