SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Fahamu Zaidi Kuhusu Perfume
Urembo

Fahamu Zaidi Kuhusu Perfume 

Manukato ndio kitu ambacho hufunga muonekano. Sio poa kabisa umependeza ila haunukii kama muonekano wako. Harufu huongeza kitu katika muonekano, inafanya uonekane unajijali na uko “put together” na wakati mwingine hukutambulisha. Ni muhimu sana kuwa makini na manukato hususani perfume.  Perfume hutofautiana harufu na muda wa kudumu. Napoongelea harufu namaanisha harufu ambayo ukiingia sehemu watu wanaweza inusa bila kukusogelea kwa karibu sana.

Aina za perfume

Eau de Perfum

Katika chupa ya perfume aina hii, manukato ( chanzo cha harufu) ni asilimia 15 hadi 20. Huchukua muda mrefu zaidi kuisha mwilini yani masaa manne hadi matano mwilini.

Eau de Toilette

Hizi uwa na manukato asilimoa 5 hadi 15, mara nyingi hudumu kwa masaa mawili hadi matatu. Hizi ndio perfume zilizoenea na kuzoeleka zaidi. Watu wengi hutumia hizi perfume.

Eau de Cologne

Zina asilimia 2 hadi 4 ya manukato na alcohol nyibgi. Hudumu kwa masaa mawili na huwa na bei ndogo ukilinganisha na zilizotangulia.

Eau Fraiche

Hizi huwa na asilimia ndogo zaidi ya manukato yani asilimia 1 hadi 3. Pia ina alcohol kidogo na maji.Hudumu kwa muda mfupi zaidi mwilini.

  • Sehemu za kupaka perfume

Kuna sehemu kadhaa unaweza kupaka au kupulizia perfume. Ila katika hizi sehemu zote unapaswa kuchagua sehemu tatu za kupulizia unapotumia perfume, si vyema kupulizia sehemu nyingi sana. Pulizia perfume kwa kiasi tu, perfume nyingi sana kwa wakati sio nzuri. Pulizia au paka perfume yako nyuma ya magoti, kwenye kiungio cha mkono na kiganja kwa mbele, mbele ya kiwiko, nyuma ya masikio/shingoni/kwenye nywele , juu ya kitovu na pembeni ya miguu. Picha inaelezea zaidi

Vitu vya muhimu kujua kuhusu perfume

  • Tunza perfume sehemu kavu isiyo na unyevunyevu
  • Ili harufu idumu zaidi, paka vaseline sehemu unayitaka kupuliza.
  • Ngozi yenye unyevunyevu hutunza manukato kwa muda zaidi hivyo paka kwenye ngozi isiyo kavu.
  • Usisugue perfume au kuifuta na mkono baada ya kupaka.
  • Kama harufu ni kali sana na unataka upate harufu kwa mbali tu basi puliza perfume hewani na kisha pita sehemu ulopulizia mara tu baada ya kupuliza.
  • Perfume zenye alcohol hukausha ngozi na nywele. Badala ya kupuliza moja kwa moja kwenye nywele basi pulizia chanuo au kitana kisha pitisha kwenye nywele kama unachana.
  • Unaweza kutumia perfume zaidi ya moja kutengeneza harufu ya tofauti.
  • Ili kujua harufu halisi ya perfume subiri ikauke baada ya kupuliza ndio uinuse.

 

Haya ndio mambo muhimu zaidi kuhusu perfume. Siku nyingine unaponunua na kuchagua perfume basi ni muhimu kuyazingatia. Kama perfume zote hizi ni kali sana kwako unaweza kutumia aina nyingine za manukato kama body spray na splash.

Imeandaliwa na @style.with.mimie

Related posts

7 Comments

  1. High 90 Peach Mintz 1g Diamonds

    … [Trackback]

    […] Read More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-perfume/ […]

  2. Puppies Puppies For Sale

    … [Trackback]

    […] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-perfume/ […]

  3. Look At This

    … [Trackback]

    […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-perfume/ […]

  4. contrato informática

    … [Trackback]

    […] Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-perfume/ […]

  5. Carpet Cleaning Normantown

    … [Trackback]

    […] Read More on that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-perfume/ […]

  6. alacabenzi cubensis temp​

    … [Trackback]

    […] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-perfume/ […]

  7. Dnabet.com

    … [Trackback]

    […] Find More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-perfume/ […]

Comments are closed.