SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Fahamu Zaidi Kuhusu Rangi Za Gel
Urembo

Fahamu Zaidi Kuhusu Rangi Za Gel 

Rangi za Gel zimechukua umaarufu mkubwa sana kwasasa hii imetokana na kwamba zimekuwa ni jibu la kilio kikubwa cha rangi kutoka mapema, rangi hizi hudumu kwa muda wa week mbili hadi tatu kama zikitunzwa vizuri, tofauti na rangi za kawaida ambazo hukaa kwa muda mchache.

Well ikiwa rangi hizi zimekuwa zikipakwa sana kwasasa kuna ambao wanazilalamikia na wale ambao wanazisifia, leo tunakuletea faida zake na hasara zake.:

Rangi ya Gel ni ipi?

Aina hii ya rangi imeundwa na methacrylate polymer, hii rangi hukaa muda mrefu katika kucha, rangi hii ni sawa tu rangi ya kawaida tofauti zake ni kwamba hii haikauki kawaida badala yake hukauka kwa kutumia ultraviolet au LED ya ultraviolet.

Faida za rangi ya Gel;

  • Hudumu muda mrefu

Kama tulivyosema mwanzo rangi hizi huchukua muda kubanduka au kutoka, wakati mwingine hazitoki mpaka pale unapozichoka na kuamua kuzitoa mwenyewe.

  • Zinakakuka kwa haraka

Sio kama rangi za kawaida zinaweza kuchukua muda mrefu kukauka na wakati mwingine design huharibika kabla ya kukauka, rangi hizi hukauka haraka kwa kutumia ultraviolet au LED ya ultraviolet.

  • Nyepesi

Ukiachana na rangi nyingine ambazo unaweza kusikia uzito kwenye kucha, rangi za gel ni nyepesi mno.

Hasara za rangi za Gel

  • Zinaweza kusabisha Cancer

Kumekuwa na report kwamba utumiaji wa kukausha rangi hizi si salama unaweza kusababisha ungonjwa wa cancer

  • Husabaisha kucha kuwa dhaifu

Rangi hizi zimekuwa zikilalamikiwa kusababisha kucha za asili kudhoofika.

  • Inaweza kusababisha maambukizo ( Infections)
  • Wataalam wengine wanadai kuwa inachukua kucha karibu wiki 6 kupona baada ya kupaka rangi ya gel

Cha kufanya endapo utapaka rangi hii ya Gel:

  • Pumzisha kucha baada ya kutoa rangi ya gel, husitoe ukapaka tena hakikisha zinapumzika kwa muda wa week kadhaa kabla ya kupaka tena rangi hii, kuzipaka mara kwa mara unazidi kudhoofisha kucha zako za asili
  • Usikae nazo muda mrefu, rangi hii inaweza kudumu muda mrefu bila ya kuharibika lakini unashaurikwa kuitoa ndani ya week mbili hadi tatu usikae nazo zaidi ya hapo, sio tu zinaweza kudhoofisha kucha kwa kukaa nazo muda mrefu bali pia zinaweza kusababisha bakteria katika kucha.
  • Nenda kwa mtaalamu kuondoa rangi hizi, inawezekana ukawa umezichoka na kuamua kutoa hii rangi mwenyewe, unashauriwa usitoe rangi hii kwa kubandua hakikisha unaenda kwa mtaalamu azitoe.
  • Paka Sunscreen kwenye vidole vyako kabla ya kuingiza vidole vyako katika ultraviolet au LED ya ultraviolet, kulinda vidole vyako na mionzi hii ya kukaushia kucha.

Well ni matumaini yetu tumekusaidia.

Related posts

1 Comment

  1. togel terpercaya

    … [Trackback]

    […] Read More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-rangi-za-gel/ […]

Comments are closed.