SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Fahamu Zaidi Kuhusu Retinol
Urembo

Fahamu Zaidi Kuhusu Retinol 

Kama ni mpenzi wa urembo utakuwa umeshakutana nayo au kusikia kuhusu retinol, Retinol inasifika kwa kuondoa mikunjo na kufanya ngozi irudi ujanan, well leo tunakuelezea kwa undani kuhusu retinol ni nini, inafanyaje kazi? na mengineyo.

Retinol ni nini?

  • Retinol ni form ya vitamin A, ambayo hutumika kama kiungo kuwekwa katika cream, serum na lotion. Retional inasaidia kupambana na chunusi pamoja na uzee.

Umri Gani Unatakiwa Kuanza Kutumia Retinol?

  • Inaaminika ngozi yako inaanza kuonyesha dalili za uzee kuanzia miaka 20, kwahio kuanzia miaka 20 au early 30’s unaweza kuanza kutumia.

Inatumika na jinsia gani?

  • Jinsia zote zinaweza kutumia retinol.

Retinol Ina Faida Gani Katika Ngozi?

  • Inaharakisha ubadilishaji wa seli (cell turnover), Inaharakisha mchakato wa ngozi yako ya asili kwakufanya cell turnover na kusababisha ngozi kufa haraka ili cell mpya zenye afya kuchukua nafasi yake.
  • Inaongeza collagen, Collagen ni protini ambayo hufanya ngozi kuwa nene na dhabiti (yenye afya).
  • Ina antioxidant properties ambayo husaidia kusaidia kupambana na radicals ambazo zinasababisha makunyanzi na madoa meusi
  • Inasaidia kupambana na chunuzi, kwakuwa ina saidia kufanya cell turnover inasaidia kupambana na kuondoa whiteheads, blackheads, chunusi na pores zilizotokana na chunusi.

Namna Ya Kutumia Retinol

  • Chukua drop moja kisha paka usoni na kwenye shingo, kama ambavyo inashauriwa unaweza kuanza kupaka mara moja kwa week, ukaongeza mara mbili kwa week unaweza kufanya hivi kwa mwezi kisha ukaanza kupaka kila siku baada ya ngozi kuzoea kipodozi.

Namna ya ku-introduce retinol katika skincare routine yako

  • Cleanse
  • Toner
  • Retinol
  • Moisturizer
  • Sunscreen

Side effects za kutumia retinol

  • Miwasho
  • Ngozi kuwa kavu
  • Ngozi kubabuka
  • Kuwa sensitive na jua

Namna ya kukabiliana na side effects za retinol

  • Anza taratibu kutambulisha retinol katika ngozi yako
  • Paka sunscreen kupunguza ngozi kuwa sensitive na jua
  • Punguza miwasho kwa kutumia soothing serums
  • Paka moisturizer kupunguza ukavu wa ngozi

Inachukua muda gani kuona matokeo ya retinol?

  • huwezi kuona matokeo ya retinol haraka huchukua week kadhaa baada ya kutumia kwa kawaida inaweza kuchukua hadi week 6 ndio uanze kuona matokeo yake.

Muda gani mzuri kutumia retinol?

  • Kwakuwa retinol inasaidia kuharakisha cell turnover na ni sensitive kwa jua muda mzuri wa kutumia ni usiku na hakikisha unapaka sunscreen kesho yake.

Tahadhari:

  • Usitumiee retinol kama unanyonyesha au ni mjamzito
  • Usichanganye retinol na C, AHA, BHA, Benzoyl peroxide or any other active product
  • Usiache kupaka sunscreen

Does Your Skin Break Out Before It Clears Up?

Namna Ya Kutambulisha Kipodozi Kipya Cha Ngozi Katika Ngozi Yako

Related posts