V Steam imekua kwenye midomo ya watu hasa wanawake kwa muda sasa, Ikiwa inasemekana ni njia nzuri ya kusafisha sehemu za siri za kike. Tumepata fursa ya kufanya mahojiano na gyverbeautyandspa ambae ametuelezea kwa uzuri kuhusu V steam
AFS: Steaming Ni Nini?
Gyver: V steam ni tradition ya zamani ambayo ilikuwa inatumika kutoka nchi za Africa,Asia etc..njia ya kufukiza uke wako kwa mvuke utokao kwenye maji yaliyochanganywa na mimea na maua maalumu ambayo lavenda ,mugwort, rosemary, wormwood,basil etc . Kazi ya mchanganyiko huu wa V steaming herbs kuponya, kurutubisha na kusafisha uke wa mwanamke na kuuacha msafi na wenye harufu nzuri..
AFS: Ulianza kusikia lini kuhusu V Steaming?
Gyver: Muda mrefu sana, nilipojifungua mtoto wangu wa kwanza mama angu aliniambia nikalie ndo ya maji ya moto ule mvuke unisaidie kupona haraka na vile vile kupunguza uchovu maana hali ilikuwa si hali.. but sikumuliza all i wanted ni kupona na kujiskia vizuri .. nilikuwa mbishi but after day 1 nililala vizuri na mwili ukanza kuachia .. na later ndo nikaaza kuifanyia research na baada nikaileta @gyverbeautyspa..
AFS: Ulishawahi kujaribu mwenyewe na matokeo yalikuaje?
Gyver: Yes before sijaanza kutumia kwa wateja nilifanya research the best herbs for yoni na nikajaribu .. kwanza nilijiskia vizuri mno inapunguza maumivi ukiwa unaingia period.. inasaidia kuwa na harufu nzuri.. ina boost libido .. na nikawapa wengine 10 na nikapata feedback nzuri..
AFS: Kwanini Mtu Afanye V Steaming?
Gyver: Kuondoa maumivu wakati wa siku zako,kuna hali ya tumbo kuuma,kuhisi kitu kinavuta kwa chini,miguu kufa ganzi etc ukiwa na tabia ya kufanya yoni steam kabla ya period kuanza utaona tofauti kubwa
AFS: Faida za V Steaming?
Gyver: ✨Husaidia kukaza misuli ya uke hivyo kubana V.
✨Husaidia mzunguko wako uwe vizuri ,
✨Husaidia kuzuia wale wenye shida ya kupata mabonge ya damu wakati wa hedhi au kupata damu nyingi hii ni shida ya hormones pia
✨Husaidia kuondoa infection zinazo jirudia mara kwa mara
✨Husaidia wenye shida ya V kuwa mkavu au kukosa hamu ya tendo la ndoa
✨Nzuri kwa wanawake wanaokaribia kufunga hedhi au menopause kusaidia kupunguza discomfort wanazo pata
✨Husaidia kuondoa harufu mbaya ,hii ni kwa wale wenye shida ya infection wakati mwingine baada ya hedhi pia unaweza kutumia kuondoa ile harufu ya mwisho
✨Ni muhimu kwa kila mzazi baada ya kujifungua inasaidia sana kurudisha V katika hali ya kawaida
AFS: Hasara za V Steaming?
Gyver: Usipokuwa makini utajiunguza na maji ya moto..pia huruhusiwi kufanya kila siku ..
Ni after period na kabla ya period kwa mwezi mara 2 au 3 kutegemea .. kama unavyojua kitu chochote ukifanya sana lazima kiwe na madhara .
AFS: Nani anatakiwa kufanya V Steaming?
Gyver ✨Mwanamke yeyote mwenye V
AFS: Nani hatakiwi kufanya V Steaming?
Gyver: Kwanza kabisa wajawazito, wanawake mjamzito hawaruhusiwi kabisa kufanya V steam. V STEAM inasababisha mimba kuaribika na kutoka .
Mwanamke ambaye ana infection kali ya V, kama UTI au fangasi kali, huyu haruhusiwi kabisa kufanya vsteam kwasababu, vsteam ni mchanganyiko wa mimea na maua yenye virutubisho na sio dawa. Tunashauri kumuona daktari, tumia dawa na utakapo maliza dawa ndo ufanye vsteam ambapo itakusaidia kuponya V haswa na kuondoa mabaki ya uchafu yaliyoachwa na infection .
Na Wanawake ambao ni bikra, hawa pia hawaruhusiwi kabisa kufanya v steam.
AFS: Kama ipo muda mrefu kwanini sasa ndio inasikika Zaidi?
Gyver:Ipo muda mrefu kweli kwanini sasa inaskikia zaidi ni utandawazi jaman dunia inaenda kasi sana so vitu vinatufikia ukingalia instagram, google etc
AFS: Je V Steaming inaweza ku-harm good bacteria or natural P/h Balance kwenye V?
Gyver: Yes uki overdo it .. na ndo maana tunashauri 2 to 3 a month .. More than that, do it at ur own risk🤣🤣🤣🤣
AFS: Chochote ambacho ungependa kuongezea kuhusu V Steaming.
Gyver: Hakikisha unanunua V- steam herbs mtu unayejua kweli huyu anauza kitu anachojua just in case unaswali unaweza kumuliza na akakujibu kwa ufasaa..
✨ Epuka kujisafisha V kwa douching au kujiingiza vidole kwenye V, hii huondoa bakteria wazuri wanaoulinda V yako na kusababisha magonjwa mbalimbali kama UTI na Yeast infections.
Fanya Vaginal Steaming kwa afya ya V yako.💃🏽💃🏽😋

Related posts
3 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Read More here to that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-v-steam/ […]
… [Trackback]
[…] Find More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-v-steam/ […]
… [Trackback]
[…] Read More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/fahamu-zaidi-kuhusu-v-steam/ […]