SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Faida 6 Za Ukwaju Katika Urembo,Afya Na Nywele
Urembo

Faida 6 Za Ukwaju Katika Urembo,Afya Na Nywele 

Wengi wetu ni wapenzi wa juice ya hili tunda na wengi tunaitumia majumbani kupunguza uzito, lakini kumbe ukwaju una matumizi mengi tofauti tofauti ukianzia kwenye afya, urembo na hata nywele.

Katika Ngozi husaidia

Katika Nywele husaidia

 • Kuzuia Kukatika Kwa Nywele
 • Husaidia kutibu ngozi ya kichwa yenye mafuta

Katika Afya Ukwaju

 • unasaidia kupunguza uzito

Jinsi ambavyo unaweza kutumia ukwaju kwa ajili ya ngozi

kungarisha ngozi 

mahitaji

 • tunda za ukwaju – 30 grams
 • maji ya moto – 150 grams
 • manjano – nusu kijiko cha chai

Namna ya kufanya

 • loweka tunda za ukwaju katika maji ya moto kwa dakika kumi
 • toa mbegu na ubaki na juice nzito ya ukwaju
 • ongeza manjano katika juice hio ya ukwaju\
 • paka mchanganyiko wako katika uso wako na uache kwa dakika 15
 • osha kwa maji ya vuguvugu

Note – mchanganyiko huu unasaidia zaidi kwa wenye sura/nyuso zenye mafuta unaweza kufanya hivi mara mbili kwa week.

Kuondoa weusi kwenye shingo 

Mahitaji

 • juice ya ukwaju nzito – kijiko kimoja
 • asali – kijiko kimoja
 • rose water – kijiko kimoja

Namna Ya Kufanya

 • changanya juice ya ukwaju, rose water na asali
 • paka mchanganyiko huu katika shingo na uuache kwa dakika 20
 • osha shingo yako kwa rose water au maji ya uvuguvugu

Fanya hivi mara moj kwa week katika kipindi cha miezi miwili utaona matokeo

Kutibu chunusi

Mahitaji

 • juice ya ukwaju – kijiko kimoja
 • mtindi – kijiko kimoja
 • manjano – kijiko kimoja

Matumizi

 • changanya mahitaji yako ( mtindi, ukwaju na manjano)
 • paka usoni na ukae nao mpaka ukauke, unaweza kuchukua dk 20-30
 • osha uso kwa maji ya vuguvugu na paka mafuta kwa ajili ya ku moisturize ngozi

Fanya hivi mara mbili kwa week sio tu itaondoa chunusi bali pia itakupa ngozi nyololo

Ukwaju Katika Nywele

Kuzuia ukatikaji wa nywele 

 

Mahitaji

 • 15 gram za ukwaju

Matumizi

 • loweka ukwaju wako katika maji acha kwa dakika 10
 • toa mbegu na upate juice ya kuwaju, paka katika nywele na ngozi ya nywele massage kwa dk kadhaa
 • tumbukiza taulo katika maji ya moto na ukamue kidogo
 • tumia taulo hili kufunga kichwa chako kikiwa bado kina mchanganyiko huo, acha mchanganyiko huu kwa nusu saa.
 • osha mchanganyiko wako kwa shampoo ukifuatiwa na conditioner

fanya hivi mara mbili kwa week kuzuia kukatika kwa nywele

Husaidia kutibu ngozi ya kichwa yenye mafuta

ngozi yenye mafuta inaweza kusababisha matatizo mengi kwenye nywele ikiwepo m’ba na kukatika kwa nywele

Mahitaji

 • juice ya ukwaju (nzito) – vijiko viwili
 • olive oil – kijiko kimoja
 • butter milk – kijiko kimoja

Matumizi

 • changanya juice ya ukwaju,olive oil na butter milk
 • paka mchanganyiko wako katika nywele na umassage kwa muda wa dk 5-10
 • acha mchanganyiko wako ukae kwa dakika 15, kama utakua unakukera vaa mfuko wa plastic
 • osha kwa kutumia maji ya vuguvugu na shampoo

rudia kufanya hivi mara mbili kwa wiki kuondoa mafuta katika ngozi ya nywele zako.

unasaidia kupunguza uzito

Mahitaji 

 • Ukwaju na maji

Matumizi

 • unaweza kutengeneza kama juice ama kuwa una weka ukwaju katika maji yako ya kunywa
 • kutumia kinywaji hichi mara mbili kwa siku unaweza kupungua uzito kwa haraka, masaa matatu baada ya kula na muda wa kulala

Note: Ukwaju una uwezo mkubwa wa kupunguza mwili, usitumie kinywaji hiki kama huna mwili mkubwa sana na kama una vidonda vya tumbo.

 

 

 

Related posts

3 Comments

 1. 대구웨딩홀

  … [Trackback]

  […] Here you will find 56889 more Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/faida-6-za-ukwaju-katika-uremboafya-na-nywele/ […]

 2. legal psychedelics in usa

  … [Trackback]

  […] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/faida-6-za-ukwaju-katika-uremboafya-na-nywele/ […]

 3. vig rx

  … [Trackback]

  […] Read More on on that Topic: afroswagga.com/urembo/faida-6-za-ukwaju-katika-uremboafya-na-nywele/ […]

Comments are closed.