SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Faida Na Matumizi Ya Mafuta Ya Bio-Oil
Urembo

Faida Na Matumizi Ya Mafuta Ya Bio-Oil 

Bio oil ni mafuta yanayosifika sana na wengi hupenda kuyatumia! Leo utajifunza faida zake kama bado hujaanza kuyatumia fanya hivyo mara moja!

  • Kuondoa Michirizi

Moja kati ya matumizi makubwa sana ya Bio-Oil ni kuondolea michirizi. Michirizi ni mistari inayotokea kwenye ngozi hususan tumboni na mapajani kutokana na ngozi kupoteza uwezo wake wa kuvutika.Matumizi sahihi ya Bio-Oil yanasaidia kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la michirizi katika ngozi

  • Kuondoa Makovu

Bio-Oil husaidia sana kuondoa makovu, hususan itakapoanza kutumika mapema mara tu baada ya kidonda au jeraha kupona.Makovu machanga hupona haraka zaidi kuliko makovu ya muda mrefu

  • Kutibu Ngozi Iliyosinyaa Na Kunyauka

Ndio. Kwa mtu mwenye ngozi iliyoanza kuzeeka au iliyozeeka basi atumie Bio-Oil. Baada ya muda sahihi ngozi yake itarejea hali ya uzuri na yenye afya 

  • Kutibu Ngozi Kavu / Iliyokauka

Bio – Oil inasaidia kuboresha afya ya ngozi na kuiwezesha iwe na maji na unyevu unyevu wa kutosha. Ngozi kavu huwahi kuzeeka, kwa hiyo matumizi ya Bio-Oil yatasaidia kuzuia ngozi kuwahi kuzeeka.

  • Kurekebisha Rangi Tofauttofauti Za Ngozi Na Kuifanya Iwe Rangi Moja


Bio-Oil husaidia kurejesha afya ya seli za ngozi na kusaidia muonekano wake mzuri. Husaidia kuondoa rangi mbaya zisizopendeza zinazotokana na athari za jua, vipodozi, kuungua nk.Matokeo yake ni kuwa na ngozi nzuri yenye kupendeza, na rangi inayofanana.

  • Bio Oil Inapatikana Wapi?


Bio-Oil hupatikana kwenye Famasi(Maduka ya dawa) na Maduka ya vipodozi.
Kuna changamoto kubwa sana ya Bio-Oil ambazo ni feki na zinapatikana kwa wingi hususan maduka ya vipodozi ambayo hayanunui kutoka kwa wasambazaji waaminifu.
Hakikisha Bio-Oil utakayonunua ni sahihi kwani ndipo utakapoona matokeo mazuri. Vinginevyo hautaona matokeo mazuri ilhali umetumia pesa nyingi sana kuyanunua.

Related posts

1 Comment

  1. ไซด์ไลน์

    … [Trackback]

    […] Read More to that Topic: afroswagga.com/urembo/faida-na-matumizi-ya-mafuta-ya-bio-oil/ […]

Comments are closed.