SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Faida Za Brokoli Kwa Afya Na Urembo
Urembo

Faida Za Brokoli Kwa Afya Na Urembo 

Broccoli ni aina ya mbogamboga ambayo inataka kufanana sana na kabeji, lakini yenyewe majani yake huwa na muonekano wa kijani sana tofauti na ilivyo kwenye kabeji.Vile vile ni tofauti na Cauliflower, cauliflower ni nyeupe Wakati broccoli ni ya kijani. 


Mara nyingi mbogamboga hii hutumiwa sana na wahindi na hata kupatikana imekuwa ikipatikana sana kwenye masoko yanayotembelewa sana na watu wa jamii hiyo. Kwa Dar es salaam Inapatikana Sokoni kisutu na Mwenge. 


Mbogamboga hizi zinapoandaliwa vizuri na kupata juisi yake huwa na manufaa zaidi na miongoni mwa faida za mbogamboga hizo ni pamoja na hizi zifuatazo:

 • Mfumo wa Neva: Inasaidia kufanya mfumo mzima wa neva kufanya kazi inavyotakiwa na kufanya ubongo kufanya kazi yake vizuri kwa kuwa ina madini ijulikanayo kama potasiamu (potassium), na kisha misuli kuwa na nguvu.
 • Msukumo wa damu: Brokoli ina potasiamu na madini chokaa kwa wingi inayosaidia msukumo wa damu kuwa sawa.
 • Inapambana na sumu :Ina Vitamic C ambayo husaidia kupambana na sumu mwilini.
 • Inalinda na kujenga mifupa: Vitamini K pamoja na Madini chokaa vinasaidia kujenga na kulinda mifupa.
 • Kuathirika na jua: Inasaidia kuondoa sumu ya kwenye ngozi pamoja na kurejesha uhalisia wa ngozi.
 • Kinga dhidi ya maradhi: Ina zinki na seleniamu ambazo zinasaidia kuifanya kinga ya mwili kuwa imara.
 • Inaimarisha afya ya Ngozi na kuchelewesha uzee. Broccoli ina virutubisho vingi muhimu vitamin c pamoja na nicotinamide mononucleotide ambacho imethibika kuwa inachelewesha dalili za uzee. 
 • Inaimarisha afya ya nywele na kupunguza kukatika kwa nywele. Broccoli ni Mboga yenye virutubisho vya afya ya nywele zako. Ongeza kwenye diet yako. 


NAMNA YA KUTENGENEZA/KUTAYARISHA

 • Unaweza kuchemsha peke yake ukazila zenyewe pamoja na supu yake (unaicha na maji maji)
 • Unaweza kuchanganya na carrots, gilgilani, cabbage ukazi steam kidogo.3. Unaweza kurost na kuku. 
 • Wale vegetarian wanapata virutubisho muhimu kwenye miili yao. Wananufaisha na kuboresha afya kwa ujumla.

Urembo ni pamoja na kula Kwa afya kwa kufanya hivyo utapata ngozi yenye afya, nywele pamoja afya ya mwili kwa ujumla.
Kama bado hujaanza kula Broccoli Anza Sasa!

©binturembo 

Related posts