Giligiliani ni kiungo cha kawaida sana,wengi tunakitumia jikoni kwenye mapishi mbalimbali,Kinaharufu nzuri na ladha ya uchachu kwa mbali.Majani na mbegu za giligiliani vyote hutumika kama viungo jikoni.Giligiliani inawingi wa Vitamini A, B6, C,B12,pia ina wingi wa madini chuma(iron),Calcium na Magnesium.


Giligiliani inasifika kwakua dawa na kinga ya magonjwa mengi.Historia inaonyesha kwamba Kiungo hiki kilitumika kama dawa tangu enzi za kale nchini Egypt. Hata hivyo,tafiti za kisayansi za karne hii ya 21 zinathibitisha taarifa hizi.


Ni vyema kujua kwamba tunaposema chakula Fulani ni dawa,basi maana yake ni kwamba chakula hicho kinavirutubisho Fulani ambavyo huweza kukabiliana na ugonjwa Fulani au laa kuupa mwili uwezo wa kukabiliana na kujikinga na ugonjwa Fulani na si vinginevyo.

Hizi ni baadhi ya faida za giligiliani katika Urembo  :


1. Huondoa chunusi na madoa kwenye ngozi.


Mahitaji

  •  Giligilani kiasi
  •  Kijiko kimoja cha Manjano (Binzari Manjano) 


Ili kuondoa chunusi na madoa meusi. Twanga au sigina majani ya giligiliani, chuja au kamua ili kupata maji yake. Pima vijiko vinne vya maji ya giligiliani kisha changanya na kijiko 1 cha chakula cha manjano(Binzari manjano).Pakaa kwenye ngozi ,acha ikauke kisha osha au nawa na maji vuguvugu.


Onyo: Usisugue ngozi paka taratibu 


Kuipa ngozi mng’ao. 

Mahitaji 

  • Giligilani kiasi 
  • Tango 1


Saga giligilani na tango pamoja upate mchanganyiko mzito, hii utatumia Kama mask. Pakaa usoni Baki nayo kwa dakika 20 Kisha Osha kwa maji ya kawaida. 
Rudia Kwa wiki Mara moja Sio zaidi ya Mara mbili. 
Mask hii Inatumika kwa ngozi aina zote Ila  ni nzuri zaidi  Kwa wenye Ngozi ya mafuta. 


Jee wewe unatumiaje giligilani kwenye Urembo!? Tuambie kwenye comment hapo chini 


Shea na uwapendao , imeandikwa na @binturembo