SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Faida Za Kitunguu Maji Kwenye Nywele
Urembo

Faida Za Kitunguu Maji Kwenye Nywele 

Mwaka jana mwanamuziki Cardi B aliandika kwenye account yake ya Instagram kwamba huwa anatumia maji ya kitunguu kuoshea nywele zake “My last 2 washes I been boiling onions and using the water to wash my hair. I used to do this 6 years ago when I started my healthy hair growth journey. I stopped cause I got really lazy. Its odorless and I notice that it’s been giving a shine to my hair (sic),”

  • Wakati Cardi yeye anatumia kupata shiny look kuna wengine ambao wanasema kutumia maji ya kitunguu kuna jaza nywele kama una nywele chache.
  • Lakini pia inaaminika kitunguu maji kinauwezo mkubwa wa kuzuia ukatikaji wa nywele
  • Kuna wanao tumia kitunguu kukuza nywele
  • Kutumia kitunguu kuondoa mba kichwani

Kwa kifupi kitunguu maji kinaaminika kuwa msaada mkuwa katika kufanya nywele zako ziwe nzuri, Je unatumiaje kitunguu maji kupata matokeo haya?

Unaweza kutumia kama steaming

  • Chukua kitunguu maji, mafuta ya castor oil kiasi weka na maji kidogo na saga kwenye blender kisha unachuja halafu osha nywele zako na shampoo unapaka hiyo steaming na unakaa nayo kwa nusu saa kisha unaosha bila shampoo unapaka mafuta yako ya nywele kila siku unaenda kusuka au kubana mtindo unaoutaka.

Unaweza kutumia kuoshea nywele

  • Cardi B yeye amesema huwa ana chemsha vitunguu, kisha anatumia maji ya kitunguu kuoshea nywele zake, na amesema ukifanya hivyo unapata mng’ao katika nywele zako.

Namna nyingine unazoweza kutumia kitunguu kwenye nywele zako

Jinsi ya kuandaa

  • Chukua kitunguu kimoja au viwili kutegemeana na ukubwa wa kitunguu chenyewe. Fuata hatua zifuatazo:
  • Osha vizuri kitunguu au vitunguu na kisha ukimenye au uvimenye
  • Kata kitunguu au vitunguu vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kusaga au kutwanga
  • Saga kwenye brenda au twanga kwenye kinu , njia yoyote ile ambayo kwako ni rahisi kwako.  Visage au vitwange mpaka vilainike kabisa ili uweze  kutoa maji kwa urahisi.
  • Ukishasaga au kutangwa vitunguu , vichuje  vizuri ili upate maji maji .Zingatia usiweke maji kwa hivi vitunguu.

Jinsi ya kupaka

Nywele sio lazima ziwe safi maana  unapaswa  kuziosha  baada ya kupaka maji ya vitunguu.

  • Chukua pamba ambayo utatumia kupaka hayo maji ya vitunguu kwenye nywele zako. Paka zile sehemu ambazo nywele zimekatika. Unaweza pia paka  kichwa kizima.
  • Baada ya kupaka  unapaswa kuvaa kofia ya plastic na kitambaa kwa juu ili kuweza kupata joto . Tahadhali usikae kwenye mashine ya steam au dryer.
  • Ukiwa na kofia ya plastic na kitambaa kwa juu ya nywele zako , ukae hivyo hivyo kwa masaa  manne hadi matano.
  • Baada ya hapo unaweza kuosha na kukausha nywele zako na kuweka style yoyote ile.

Hitimisho

Ni vema kufanya zoezi hili la kupaka vitunguu walau mara mbili kwa mwezi. Ikiwa harufu ya kitunguu ni kali, unaweza weka asali kidogo kwenye maji ya vitunguu.

Lakini pia hakikisha hauna allergy na kitunguu na pia kama utapaka utapata miwasho basi usiendelee kutumia.

Related posts