SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Faida Za Red Wine Katika Ngozi Na Nywele
Urembo

Faida Za Red Wine Katika Ngozi Na Nywele 

Hakuna kitu kina kufanya ujisikie vyema baada ya siku ndefu na uchovu kama kukaa sehemu tulivu ukiwa unakunywa mvinyo (wine), ukiachana na kukufanya u-relax lakini pia mvinyo unafaida katika nywele na ngozi yako. Leo tunakupa faida 5 unazozipata kutokana na kunywa red wine.

  • Kupambana na chunusi

Mvinyo mwekundu una resveratrol ambayo hupunguza ukuaji wa bakteria inayosababisha chunusi. Kunywa glasi ya mvinyo pia inaweza kuzuia kuenea kwa keratinocyte ambayo inahusika na kusababisha vidonda vya chunusi. Watu wengine pia wanaamini kuwa kutumia red wine kwa kupaka usoni kunaweza kukusaidia husafisha pores.

Mambo Matatu (3) Ya Kuzingatia Ili Kupata Kipodozi Kinachoifaa Ngozi Yako

  • Kung’arisha Ngozi

Unataka ngozi inayong’aa na nzuri asili? Jiagize glasi ya mvinyo mwekundu pale utakapokwenda kunywa vinywaji. Polyphenols katika red wine hubadilisha (Kutoa ) rangi dhaifu na kusaidia kukupamng’ao katika ngozi yako. Inasaidia pia kuondoa stress katika mwili wako na kuzuia uharibikaji wa ngozi unaotokana na stress hizo. Lakini pia kupaka mvinyo huu mwekundu moja kwa moja kwenye uso wako na kusugua kwa dakika chache pia kunaweza kufanya ngozi yako kung’aa.

  • Inapunguza ngozi kuaribuwa na jua

Ingawa haiwezi kuchukua nafasi ya sun screenjua, red wine ina vioksidishaji na asidi ya amino, ambayo ina kizuizi cha asili kwenye ngozi yako na kuilinda kutokana na miale yenye nguvu ya UV ya jua. Lowesha pamba kwenye red wine paka juu kwenye sehemu iliyoathiriwa na kuchomwa na jua kunaweza kupunguza hali ya kuchomwa na jua na kuponya eneo lililoathiriwa haraka.

Umuhimu Wa Kupaka Sunscreen Katika Ngozi

  • Kusaidia Ukuazi Wa Nywele

Kunywa red wine pia kunahusishwa na kuboresha mzunguko wa damu mwilini, pamoja na kichwa. Hii inasaidia ukuzaji na ukuaji wa nywele na kuzuia upotezaji wa nywele. Unaweza pia suuza nywele zako na mvinyo mwekundu. Baada ya kuosha nywele zako na shampoo suuza nywele na mvinyo mwekundu hii itasaidia kukupa nywele zenye afya na zinazong’aa

  • Husaidia Kukarabati nywele zilizoharibiwa

Mvinyo mwekundu una virutubisho ambavyo husaidia kukarabati nywele ambazo zimekatika au kuharibiwa na moto. Changanya mvinyo mwekundu na maji kisha suuza nywele zako kuanzia kwenye shina mpaka kwenye ncha.

wakati mwingine ukikaribishwa red wine usikatae.

 

Related posts

2 Comments

  1. pg slot

    … [Trackback]

    […] Find More Info here to that Topic: afroswagga.com/urembo/faida-za-red-wine-katika-ngozi-na-nywele/ […]

Comments are closed.