SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Fursa Katika Sekta Ya Urembo Zinazoweza Kukutajirisha
Urembo

Fursa Katika Sekta Ya Urembo Zinazoweza Kukutajirisha 

So linapokuja suala la ujasiriamali hususani kwenye masuala ya urembo basi waafrika na hususani Bongo tupo nyuma sana. Inawezekana tatizo ni kipato lakini pia kuna uwezekano hatujui fursa kubwa iliyopo kwenye urembo ndio maana kila siku kuna vitu vipya vinazinduliwa lakini tunaishia kuvisikia kwa watu na nchi baki ila sio kwetu.

Hizi ni baadhi tu ya fursa zinazoweza kubadili maisha yako ikiwa zitatumika vizuri.

  • Permanent Makeup (Makeup ya kudumu)

Ni jambo la ajabu sana kuona nchi jirani zina wataalamu wengi wa permanent make up lakini kwetu ni ishu. Hapa siongelei wachora tattoo japo makeup hizi ni kama tattoo flani. Katika sekta hii kuna wataalamu wa make up za kudumu milele na za kudumu kwa miaka kadhaa. Mtaalamu hutoa huduma za kumpaka mteja wanja, lipstick, lip liner,concealer ya kudumu na kadharika. Kumekua na mafuriko ya wataalamu wa micro blading kwenye nchi nyingi, hii ni sanaa inayohusisha kuchora alama mfano wa nyusi ili kuzipa nyusi ujazo lakini cha ajabu sisi bado tumekatalia kwenye kuchora wanjaa wa tattoo unaoacha nyusi zikionekana kama vile zimechorwa na marker pen.

Kwa wastani, mteja mmoja wa nyusi (micro blading) anaweza kupata huduma kwa gharama ya shillingi laki mbili au zaidi. Mdomo hugharimu zaidi. Bei ya seti ya vifaa vinavyotakiwa kutumika kwa mteja mmoja ni kama elfu sitini au chini zaidi. Kwa mtu anayejiweza kuna vifaa bora zaidi vinavyogharimu zaidi, kudumu zaidi na kutoa matokeo zaidi. Kwakuwa wasanii wa make up za kudumu ni wachache kuna uwezekano mkubwa wa kupata wateja wengi sana. Ukipata wateja kumi kwa mwezi basi una million mbili, ukitoa gharama una uhakika wa kubaki na faida isiyopungua million moja kwa wateja kumi tu wa nyusi. Ili uanze biashara hii ni muhmu kujifunza au kupata course mtandaoni, baadhi ya site hutoa vyeti pia. Pia kuna watu ambao hutoa mafunzo kupitia youtube na mitandao mingine ya kijamii.

 

  • Natural skin products (Bidhaa asili za ngozi)

Kuna uhaba mkubwa wa bidhaa asili zisizokuwa na madhara, bidhaa nyingi hususani zinazouzwa mtandaoni ni mchanganyiko wa bidhaa kadhaa zenye kemikali zinazodhuru ngozi. Wauzaji hudai hazina madhara lakini ni dhahiri kuwa si vitu vizuri maana hata ingredients za bidhaa huwa haziwekwi kwenye bidhaa hizo. Kila siku tunakutana na watu walioathiriwa na vipodozi haramu.

Bidhaa asili uwa na bei ghari kutokana na ubora na faida ya kutokuwa na madhara kwenye mwili. Baadhi ya bidhaa asili zinazoweza kupata soko kubwa ni bidhaa za kubadili rangi ya ngozi, scrub, skin building oil kwa watu ambao ngozi zao zimekuwa nyepesi kutokana na cream, exfoliating lotion (lotion zinazoondoa ngozi iliyokufa), mafuta ya kuondoa sugu, sunscreen. Ukiweza kutengeneza bidhaa nzuri zinazoleta matokeo kweli basi utapata wateja wengi. Nimeona watu wakiuza scrub ya sukari na vannilla kwa elfu hamsini japo gharama zake hazijazidi hata elfu 15000. Cha msingi ni kufanya uchunguzi, jua soko lako, buni na tengeneza bidhaa nzuri zinazofanya kazi kweli na jitangaze.

  • Kuagiza na kuuza bidhaa mpya za urembo

Kuna vitu vingi tunakutana navyo mitandaoni kila siku lakini ukizunguka madukani kuna mawili; hukipati au unakipata kwa bei kubwa mno. Kuna vitu kama urembo na mawe ya kubandika kwenye kucha, vibanio vya weaving, lens za macho, wanja unaodumu muda mrefu, vifaa vya urembo vya umeme, na vitu vingine vigeni unavyokutana navyo kwenye mitandao. Mara nyingi bidhaa ikitoka nchi zinazoendelea huwa za mwisho kufikiwa hivyo kuwa wa kwanza kuagiza na kuteka soko. Unapokuwa wa kwanza kuingiza bidhaa ni rahisi kujipangia bei na kupata wateja zaidi.

 

  • Body modifications (kubadili maumbile)

Anha anhaaa hapana, sio zile lotion zinazouzwa mtandaoni. Zile wote tunajua ni za uongo, japo watu wamepiga pesa kweli lakini huo ni utapeli. Hapa naongelea surgey na matumzi ya vifaa mbalimbali kubadili muonekano. Nchi rafiki kama Kenya, South Africa, Ghana na Nigeria wameshachangamkia fursa kama kawaida yao japo hata wao hawajachangamka vya kutosha. Karibia kila mwanamke ana kitu anatamani angeweza kubadili. Kila siku watu wanatapeliwa kwa kuuziwa bidhaa zinazotoa matumaini ya uongo. Hii ni fursa kubwa. Ili ufanye haya unahitaji kujifunza namna ya kutoa huduma hizi au kuwa na akili ya kuweza kupata wawekezaji.

Kujifunza itahitaji kujitoa sana na elimu ya udaktari lakini kuwekeza kwenye hii fursa au kutafuta wawekezaji inawezekana. Haitakuwa rahisi lakini kikubali basi ni kitu kinachoweza kubadili maisha yako na wenzako. Unaweza pitia kurasa kama @grandvillemedlaser kuona mfano wa ninachokiongelea. Procedure moja ndogo huweza kugharimu kwanzia millioni mbili, lakini ni watu wengi wako radhi kutoa pesa mara kumi ya hiyo ili tu wapate muonekano wanaotaka

  • Kubuni na kutengeneza nguo za kuogelea

Inahsangaza sana, hivi hata nguo ndogo ndogo kama bikini hatuwezitengeneza? Je vikaptula laini vyenye bra zake au vest kwa ajili ya watu
wasiopenda kuacha sehemu kubwa ya mwili wazi. Kila mtu anakimbiliakubuni mavazi makubwa lakini kuna fursa katika kubuni mavazi ya ufukweni
kwa ajili ya mwanamke wa kiafrika, yatakayohifadhi mwili wa kibantu vyema. Mavazi ya ufukweni ni madogo lakini mara nyingi bei zake huwa juu
kidogo. Pisi chache zinaweza kukuingia faida kubwa.

  • Personal shopper (Mnunuzi wa mavazi kwa niaba ya wengine)

 

Kuna watu wanapenda kupendeza lakini hawajui wavae nini, wavae wapi, wanunue wapi na wengine hawana muda wa kuzunguka wakitafuta mavazi na nakshi. Hapa ndipo umuhimu wa personal shopper unakuja. Kama una imani unajua vizuri kuvaa na kupangilia mavazi, unajua namna ya
kuongea na muuzaji hadi ukafikia bei nzuri unayoweza imudu na unajua sehemu ambazo mavazi mazuri hupatikana basi hii fani inaweza
kukufaa. Si lazima uwe na sifa zote kuna vitu vingine unaweza kujifunza taratibu. Iliufanikiwe katika hii fani inabidi uwe na aina fulani ya wateja wengi wakiwa wa kipato cha kati na kipato cha juu. Malipo hutegemea muda unaotumia, idadi ya manunuzi, tukio na idadi
ya huduma atazopata mteja kama ushauri, manunuzi na elimu kama upakaji wa makeup. Unaweza kujipatia kiasi cha chini zaidi cha laki moja kutoka kwa mtu mmoja unapotoa huduma ndogo zaidi. Hakuna kizuri kinachokuja bila kujituma na kujitangaza. Fursa ni nyingi sana, hizi ni baadhi tu. Chukua muda wako kuchunguza zaidi unaweza kubahatisha fursa itakayobadili maisha yako kabisa kama ukiifanya lwa kuzingatia.

Article Imeandikwa na @Raymimie

Related posts

2 Comments

  1. magic chocolate bars

    … [Trackback]

    […] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/fursa-katika-sekta-ya-urembo-zinazoweza-kukutajirisha/ […]

  2. polka dot candy bar

    … [Trackback]

    […] Find More here on that Topic: afroswagga.com/urembo/fursa-katika-sekta-ya-urembo-zinazoweza-kukutajirisha/ […]

Comments are closed.