SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Hatua 8 Za Kufanya Ngozi Yako Ionekane Kijana Daima
Urembo

Hatua 8 Za Kufanya Ngozi Yako Ionekane Kijana Daima 

Kuwa na ngozi yenye muonekano mzuri ni jambo la kujivunia kwa watu wa rika zote hapa duniani. Watu huwa wanatumia kiasi fulani cha kipato chao kwa ajili ya kutunza wa ngozi zao. Hivyo ni vyema ukawa na ufahamu sahihi wa jinsi gani ya kutunza ngozi yako ili isizeeke mapema. Hizi ni baadhi ya njia za kuitunza ngozi yako;
  • Hakikisha unaepuka mionzi ya jua kwa kadri inavyowezekana( Protect yourself from the sun).
Hii ni njia muhimu sana ya kuitunza ngozi yako ambayo si lazima uwe na pesa ,bali ni kuwa na uelewa sahihi na baadaye kubadilisha mtindo wa maisha. Kwa mtu ambaye hakuepuka mionzi ya jua kwa miaka mingi katika maisha yake anaweza akapata saratani ya ngozi, lakini pia ngozi hujikunja mapema(wrinkles),madoa meusi(black spots) na matatizo mengine ya ngozi.
  • Fanya hivi kupunguza mionzi ya jua kama lazima ufanye kazi wakati mchana;
Tumia vipodozi vinavyozuia mionzi ya jua(use sunscreen)
Vaa mavazi yanayofunika sehemu kubwa ya mwili, pia hapa ni muhimu kuvaa kofia
Penda kukaa kwenye kivuli(find a shade)
  • Acha kuvuta sigara( Don’t smoke).
Uvutaji wa sigara unafanya ngozi yako ijikunje na kuzeeka mapema. Hii ni inatokana na kwamba uvutaji wa sigara unafanya mirija iliyo midogo katika sehemu ya nje ya ngozi kuwa na uwazi mdogo(narrowing cutaneous blood vessels) na hivyo kupelekea hewa ya oksijeni na virutubisho muhimu kutotosha kwa ajili ya afya ya ngozi. Licha ya sababu hapo juu,pia uvutaji wa sigara inaharibu ‘elastin’ na ‘collagen’ ambavyo kwa pamoja hufanya ngozi kuwa imara.
Haishii hapo tu,jinsi unavyo ukunja uso wako wakati wa kuingiza moshi(repetitive facial expressions)  hupelekea mikunjo katika ngozi(wrinkles).
Kama unaipenda ngozi yako ni bora ukaacha kuvuta sigara. Ni vyema ukamwona daktari ili ukushauri ni jinsi gai unaweza kuacha kuvuta sigara.
  • Hakikisha unatumia matunda na mboga za majani kila mara
Matunda yenye vitamin C ni muhimu sana, kwani vitamini C huzuia ngozi kuzeeka mapema  nahii hutokana na uwezo wake wa kuzuia ‘cell’  za ngozi kuharibiwa na sumu ambazo ni ‘oxidants, kwa hiyo ni anti oxidant  nzuri. Haya matunda ni kama machungwa,limao nk.
Pia matunda yenye vitmin E ni muhimu katika ustawi wa ngozi, haya matunda ni kama Carrots  nk.
Pia mboga za majani ni muhimu sana katika ustawi mzuri wa ngozi,kuna baadhi ya tafiti zinaonesha kwamba watu wanaotumia mboga za majani kila mara ni vigumu sana kwao kupata saratani ya ngozi katika maisha yao.
  • Hakikisha unapata usingizi wa kutosha
Unapopata usingizi wa kutosha ndipo hata ngozi hujiweka vizuri na hivyo kuwa na muonekano mzuri.
  • Usafi binafsi wa mwili(personal hygiene).
Wataalam wanashauri ni vyema kuisafisha ngozi yako mara mbili kwa siku wakati wa asubuhi na usiku,pia unapokuwa umetokwa na jasho,Hapa  unatakiwa uwe ‘gentle’, pia usitumie sabuni kali, ila tumia sabuni za kawaida za kuogea ‘mild soap’ haswa kwa watu wenye ngozi yenye mafuta. Pia hakikisha unatoa ‘make up’ zote kabla hujalala. Hakikisha kitanda chako na mito ni safi daima.
  • Kunywa maji ya kutosha kwani ngozi inahitaji maji
  • Fanya mazoezi kila siku
Mazoezi yanafanya mzunguko wa damu uwe mzuri na hivyo kufanya ngozi kuwa na ustawi mzuri.
  •  Tumia vipodozi vizuri kiafya vinavyoendana na ngozi yako(safe cosmetics for your body).
Kuna baadhi ya vipodozi ambavyo ni vikali sana na ukivutumia vinakupatia matokeo unayo yataka kwa muda mfupi lakini kiukweli ni hatari sana kiafya kwa hapo mbele,madhara yake ni kama ngozi kuwa nyembamba sana isiyoweza kuulinda mwili vizuri,ngozi kuzeeka mapema na saratani ya ngozi.
Hivyo chagua vipodozi vinavyooendana na ngozi yako, hivyo kama ngozi yako ni kavu tumia vipodozi vinavyoendana na ngozi hiyo na kama ina mafuta tumia vipodozi kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.
Hizi ni baadhi ya njia za kuifanya ngozi yako ionekane vizuri daima.
Habari hii ni kushea na umependae, Unasubiri nini!?
Imeandaliwa na Kuandikwa na @binturembo

Related posts

2 Comments

  1. Buy DMT Powder Online Perth

    … [Trackback]

    […] Here you can find 30602 additional Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/hatua-8-za-kufanya-ngozi-yako-ionekane-kijana-daima/ […]

  2. prescription weight loss pill phentermine​

    … [Trackback]

    […] Here you will find 14504 more Information to that Topic: afroswagga.com/urembo/hatua-8-za-kufanya-ngozi-yako-ionekane-kijana-daima/ […]

Comments are closed.