SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Historia Na Madhara Ya Lipstick Kwa Wanawake
Make Up

Historia Na Madhara Ya Lipstick Kwa Wanawake 

Lipstick ni aina ya vipodozi vyenye rangi mbalimbali vinavyotumika kupaka katika midomo hasa ya wanawake ili kuongeza urembo na mvuto wao. Historia ya kupaka rangi kwenye midomo kwa kusudi la urembo inaonyesha kuwa jambo hili lilianza zamani sana na inasemekana kuwa lilianzia huko Misri .

Ingawa matumizi ya rangi ya kupaka midomoni katika siku zetu inaweza kuwa na makusudi tofauti na yale ya zamani na kupendwa na wasichana au wanawake wa kisasa wanaokwenda na wakati katika urembo, lakini bado ni muhimu kuangalia athari zake kwa afya ya jamii na mwili wa mtumiaji mwenyewe.


Vipodozi hivi hutengenezwa kutokana na viambato mbalimbali na inasemekana kuwa baadhi ya viambato hivyo si salama kwa afya. 
Watafiti wa mambo ya afya ya jamii wanasema kuwa wanawake wengi wanaotumia rangi za kupaka midomoni wanachoangalia zaidi ni urembo na mvuto wao na wanasahau kuangalia upande wa pili wa athari zake kwa afya zao.


Katika utafiti uliofanywa huko Marekani na US Consumer Group “Campain for Safe Cosmetics” Oktoba 2007, ripoti yao iliyopewa jina la “A Poison Kiss, the Problem of Lead in Lipstick” (Busu lenye sumu) ilionyesha kuwa lipstick nyingi karibu theluthi moja, zilikuwa na madini ya ‘lead’ kwa kiwango kikubwa zaidi ya kile kilicho salama kwa afya ya binadamu.
Viambato vingine vyenye madhara ambavyo vinapatikana katika rangi hizi kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari za afya ya jamii ni pamoja na Butylated Hydroxyanisole (BHA), Coal tar (petroleum) na aluminum (Lakes color).

Pichure By @cherie_mals


Lakini pia ndani ya rangi za kupaka mdomoni kuna rangi ya Carmine au natural red 4, rangi inayotokana na wadudu wekundu waliokaushwa na kusagwa kama vile ‘Red Beetles’. 
Pamoja na rangi hii, baadhi ya vipodozi hivi pia huongezewa mafuta ya nguruwe au mafuta ya ubongo wa ng’ombe kama malighafi za kutengenezea vipodozi hivi ili viweze kulainisha midomo. Watengenezaji wengine huongeza rangi za magamba ya samaki pamoja na mazao ya mimea kama vile red beets na bizari. Mdudu RED BEETLE anaye tumika kutengenezea Lip stick

 • MADHARA YA MATUMIZI YA LIPSTICK.


Wanasayansi wanaongeza kusema kuwa viambato vyenye madhara katika rangi za kupaka midomoni vinaweza kuingia mwilini au kumezwa na kusababisha athari za kiafya kama vile saratani (kansa), magonjwa ya figo, shinikizo la damu, uchovu wa mwili usiokuwa na sababu bayana, kukosekana kwa usawaziko wa kihisia (mood swing), maumivu ya kichwa, kichefuchefu, magonjwa ya ngozi, kupasuka kwa midomo (cheilitis) na magonjwa ya neva.

Matatizo mengi ya kiafya yanayosababishwa na rangi hizi, hayatokei kwa haraka na ni mara chache sana waathirika wa rangi hizi kuhusisha utokeaji wa magonjwa wanayopata na mtindo wao wa maisha wa kutumia vipodozi hivi.


Wanawake wajawazito wanaotumia vipodozi hivi, huwaweka watoto wao walioko tumboni katika hatari ya kupata magonjwa wa mtindio wa ubongo na matatizo ya akili [Utaahira].
Sumu ya lead inayopatikana katika baadhi ya vipodozi hivi hupita katika kondo la nyuma na kufika katika ubongo mchanga wa watoto walioko tumboni na kuathiri maendeleo ya ubongo na akili za mtoto, na matokeo yake ni kuzaa mtoto asiye na uwezo wa kuelewa kile anachofundishwa kwa haraka.


Wasichana na wanawake wanashauriwa kujiepusha na matumizi ya rangi hizi kwa ajili ya kulinda afya zao. Lakini kama hakuna njia nzingine zilizo salama zaidi za kukamilisha urembo wako, unashauriwa kuepuka kujilambalamba midomo pale unapokuwa umepaka rangi hizi mdomoni.Hii hupunguza kiasi cha viambato hatarishi vinavyoingia mwilini kwa njia ya kumeza, ingawa kiasi kingine kinaweza kupenya kupitia katika ngozi laini ya midomo na kuingia ndani ya damu.

Tumia lipstick kwa uangalifu, Shea na uwapendao. 
©binturembo 

Related posts

4 Comments

 1. browse around here

  … [Trackback]

  […] Find More to that Topic: afroswagga.com/urembo/historia-na-madhara-ya-lipstick-kwa-wanawake/ […]

 2. เซ็กซี่บาคาร่า

  … [Trackback]

  […] There you will find 1053 more Information on that Topic: afroswagga.com/urembo/historia-na-madhara-ya-lipstick-kwa-wanawake/ […]

 3. Residual income opportunities

  … [Trackback]

  […] Info on that Topic: afroswagga.com/urembo/historia-na-madhara-ya-lipstick-kwa-wanawake/ […]

 4. website

  … [Trackback]

  […] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/historia-na-madhara-ya-lipstick-kwa-wanawake/ […]

Comments are closed.