Tunadhani ni wakati wa sisi kusema “Finally we can all be human”, miaka michache nyuma ilikuwa si kawaida kuona watu maarufu au models wakiwa na makosa, yaani kila mtu alitaka kuonekana perfect katika jamii, kuanzia kichwani mpaka miguuni hakuna ambae aliyetaka kuonekana na kasoro na hii ni kutokana na jamii kutaka waonekane hivyo.
Watu maarufu wengi walikuwa wakifanya plastic surgery kubadilisha mionekano yao waonekane bora zaidi, lakini kuanzia mwaka jana tumeona wengi wao wakiamua kurudi katika miili yao ya kawaida ( YASS). Na baada ya haya kufanyika tunaanza kuona brand mbalimbali nazo zikianza kutumia models wanene, ambao wana makovu, ambao meno yao hayako sawa na hii ni kufanya kila mmoja wetu aweze kujisikia huru kutumia bidhaa zao lakini kujua pia kwamba we are all human na hakuna mkamilifu.
Brand ya Gucci Beauty imerudi baada ya miaka mitano kuwa kimya, na wamerudi na lipsticks na ad campaign yao inaonyesha kuwavutia watu wengi kutokana na kutumia baadhi ya models wakiwa na mionekano ya kawaida kama binadamu wengine, kama vile lips nyembamba tulizoea kuona kila brand ya lipstick inatumia models wenye lips nene, lakini Gucci wamekuja kitofauti. Lakini pia wametumia models wenye meno ambayo hayako perfect sivyo kama ambavyo tumezoea kuona wakiwa na mpangilio mzuri wa meno na meupe.
Wakati Fenty Beauty by Rihanna, hii brand tunaweza kusema ni leading diversity brand kwa sasa, anatumia kila aina ya models, from black, wazee, wanene n.k, ukiachana tu na kutumia models wa tofauti tofauti lakini pia katika collection zake ana bidhaa za kila aina na kila rangi, kama ambavyo tunajua brand nyingi za urembo zilikuwa zikilalamikiwa kwa kukosa bidhaa za watu weusi sana au watu wanene Riri said “she is here to help”.
Katika campaign yake mpya Rihanna amemtumia huyu model ambae ana scars na hawakuzi edit kuzitoa wamemuacha kama alivyo & every ame fall in love na hii ad, well take our coins sis.
As fashion and beauty ambassador tunasema we are proud kuishuhudua hii generation ya kuwaonyesha wengi kwamba you can be imperfect perfect kwa maana tunaona namna ambavyo watu wengi wakihangaika kupata mionekano fulani, na kuhasau vingi vizuri walivyo navyo kwa kutaka kurekebisha vile vichache walivyo kosa huku wakisahau kwamba “hakuna mkamilifu”
Related posts
3 Comments
Comments are closed.
HOT TOPICS
Subscribe for newsletter
* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!
Interviews
Fahamu Zaidi Kuhusu Vazi La Vijiko Kutoka Kwa Harmonize
Mwanamuziki Harmonize ametoa wimbo wake mpya uitwao Attitude, katika music video ya wimbo huu Harmonize ameonekana akiwa amevalia vazi la leather lenye vijiko, uma na visu ( silverware/ cutlery ) Vazi hili limeonekana ku-trend sana wengine wakiwa wanalisifia na wengine kuliponda, tumemtafuta stylist na mbunifu…
Maoni Ya Mbunifu Elisha Red Label Kuhusu Event Ya Miss Tanzania 2020
Tanzania imepata mlimbwende wake mpya ambae ataenda kuliwakilisha Taifa mwakani katika mashindano ya Dunia ya urembo. Tumeona sio mbaya kama tukifanya mahojiano na baadhi ya wabunifu, makeup artist na stylist ambao wametupa maoni yao kuhusu event hii. Hapa tunae mbunifu mkubwa wa mavazi ya kike…
Meet Eddie A Young Male Makeup Artist In A Female Dominated Industry
Anaitwa Eddie ( Makeup By Eddie ) ni mvulana ambae anafanya vizuri katika tasnia ya urembo, Eddie ni makeup artist tofauti na wengine Eddie yeye ni mvulana na kama ambavyo tunajua tasnia hii imetawaliwa sana na wanawake katika bara letu la Africa. Tumepata kujua mawili…
Husiyo Yajua Kuhusu Vaazi
Weekend hii tuliweza shuhudia maonyesho ya mavazi katika Tanzania Summer Festival iliyofanyika pale Double Tree Hotel. Tulivutiwa sana na kazi ya mbunifu chipukizi [pia stylist Vaazi na hivyo kuongea naye mwawili matatu juu ya kazi zake. AFRO: Umetambulika kama stylist anayechipukia na kufanya vizuri, waweza…
… [Trackback]
[…] Info to that Topic: afroswagga.com/urembo/imperfection-is-the-new-perfection/ […]
… [Trackback]
[…] Read More Information here on that Topic: afroswagga.com/urembo/imperfection-is-the-new-perfection/ […]
… [Trackback]
[…] Find More on that Topic: afroswagga.com/urembo/imperfection-is-the-new-perfection/ […]