SUBSCRIBE NOW

* Afromate kuwa wakwanza kupata updates zetu za kila siku!

Trending News

Subscribe Now

* You will receive the latest news and updates on your favorite celebrities!

Trending News

Indian Home Remedy Inayoweza Kukusaidia Kuondoa vichwa vyeusi “blackhead”
Urembo

Indian Home Remedy Inayoweza Kukusaidia Kuondoa vichwa vyeusi “blackhead” 

Asili ya home remedy hii ni India. Ni nzuri kuondoa vichwa vyeusi “blackheads”  Blackheads /Closed comedone ” vichwa vyeusi”

Ni Aina ya Chunusi ambayo hutokea baada ya kuongezeka kwa sebum na Ngozi iliyokufa. Kama katika kuongezeka huku kwa sebum na seli za ngozi zilizokufa, kijitundu cha kinyeweleo kitakuwa wazi, hali inayoitwa open comedone au blackhead itatokea.


Kuzidi kuongezeka kwa mafuta kutoka sebacious glands, kutalifanya eneo linalokizunguka kijitundu cha kinyweleo kuvimba. Blackheads zinaweza kuambatana na mashambulizi ya bakteria wa P.acnes endapo wataweza kushambulia eneo linalozunguka kijitundu cha kinyweleo.


Tumia pilipili manga / pilipili Mtama na maziwa mtindi kuondoa blackheads “vichwa vyeusi”

Mahitaji

  • Vijiko 2 vya maziwa mtindi Kijiko 1 cha pilipili manga “pilipili Mtama” ( ya unga ni bora zaidi) 
  • Muda wa kuandaa : Dakika 1
  • Maelekezo 1. Changanya mahitaji yote kwenye bakuli safi 2. Osha uso wako, uache ukauke kidogo tu. 3. Paka mchanganyiko wako usoni na shingoni 4. Sugua taratibu kwa kuzunguka kwa dakika 55. Osha na maji ya uvuguvugu na ujikaushe. 
  • Pilipili manga inauwezo wa kuongeza mzunguko wa Damu kwenye Ngozi yako ya uso, hivyo basi mzunguko wa hewa safi pamoja na virutubisho huongezeka. Vile vile inazuia bacteria hatarishi wasiingie kwenye Ngozi yako ambao huleta chunusi aina ya blackheads “vichwa vyeusi “
  • Maziwa mtindi yana lactic acid yenyewe inaweza kutoa Ngozi iliyokufa “dead skin” na kupunguza ukubwa wa tundu za uso na kung’arisha uso wako na kuua bacteria hatari Huku ikikuachia bacteria salama Kabisa. 
  • Kila nikihisi ngozi yako kuchoka Fanya hii, blackheads zitaisha. 


Tahadhari : Pilipili manga/ pilipili Mtama inawasha. Uwasho Ndio unafanya niliyoeleza Hapo juu. Vumilia ukitaka uzuri Shart uzurike ati. 
Unatakiwa kufanya mara 1 sio Zaidi ya Mara 2 kwa wiki. 
Shea na uwapendao! 


©binturembo

Related posts